Ukurasa wa Nyumbani
Kujitayarisha
Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
Deutsch
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Português
Română
Српски / Srpski
Türkçe

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya Kwanza

Hakuweka Jarida

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Kebede alikuwa mratibu mzuri ajabu. Wanakijiji kimoja walitaka kusambaziwa maji safi, naye alifahamu shirika la kimataifa lisilo la kiserikali ambalo lingelipia baadhi ya gharama za shughuli hiyo. Alipanga mkutano kati ya viongozi wa kijiji na hilo shirika lisilo la kiserikali na kuhakikisha kwamba hakuwafanyia wanakijiji mipango yote ya mradi huo.

Watu wa kijiji chengine walitaka shule, naye alimfahamu mtu kutoka wizara ambaye angepata fedha kwa ajili ya vikundi vya kujisaidia ambavyo vilitaka kujenga shule. Kupitia kwa Wilaya, wanakijiji walijawa na furaha na kumwuliza Kebede awaongoze ili wafanikishe miradi ya kijiji chao. Wilaya ilijaa shughuli.

Kebede hakubeba daftari. Hakuandika maelezo ya yale aliyoyafanya wala tofauti za vijiji. Alisahau kwamba kijiji cha Hailitown kilikuwa na usambazaji mzuri wa maji safi na wanakijiji walishangaa kuona maafisa wa serikali wakikagua mahitaji yao ya maji. Wengi wa wanakijiji cha New Bede walikuwa wa dini ya Kiislamu na hawakupendezwa kumuona mwanamke aliyevaa nguo ambayo haikufunika mikono yake akijadiliana nao kuhusu mahitaji yao ya kielimu. Walihitaji usambazaji wa maji. Kwa muda, Wilaya ilichanganyikiwa, watu wakakata tamaa, hawakumsikiliza Kebede na uhamasishaji ukafikia kikomo.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2014.11.27

 Ukurasa wa nyumbani
Kujitayarisha