Ukurasa wa Nyumbani
Kujitayarisha
Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
Deutsch
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Português
Српски / Srpski
Türkçe

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya pili

Hakufahamu malengo yake

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Faith alikuwa na shughuli nyingi. Kulikuwa na vijiji saba Wilayani ambavyo alivihudumia. Aliendesha pikipiki yake ya magurudumu manne kutoka kijiji kimoja hadi kingine, safari iliyokuwa ndefu na ya kuchosha

"Hawa watu hawaheshimu elimu", alisema mkuu wa wilaya. "Ningependa uwawezeshe ili wapeleke watoto wao shuleni"

Jinsi alivyokwenda kijiji hadi kijiji, aliongeza hotuba ya kuwahimiza watu wapeleke watoto wao shuleni

"Hawa watu wangali wanaabudu mashetani", alisema muhuburi. "Ningependa wahudhurie Kanisa"

Kwa hivyo aliongeza hotuba ya kuwahimiza waende kanisani. " Hawa watu hawazingatii usafi", alisema muuguzi. Kwa hivyo akaongeza hotuba kueleza watu wasafishe mikono yao na kutumia vyoo. Hali hiyo ikaendelea; Mkuu mwingine yeyote alipotoa maoni kwa wanakijiji kufanya hili ama lile, Faith aliongeza hotuba nyingine kwenye ratiba yake. Mwisho wa mwaka, hakukuwepo na kituo cha jamii kilichokuwa kimejengwa au kurekebishwa

"Kwa sababu gani?" aliuliza Faith

"Sisi hukusikiza kila unapotutembelea", walisema wanakijiji, "Lakini hukujaribu hata kutusaidia kutenda tuliyoyataka"

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2013.11.15

 Ukurasa wa nyumbani
Kujitayarisha