Ukurasa wa Nyumbani
Kujitayarisha
Tafsiri:

Català
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Српски / Srpski
Türkçe

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya Tano

Hakufahamu dhana za msingi

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Paul hakumakinika wakati wa mafunzo kuhusu dhana za msingi. Hakufahamu kwamba uhamisho wa fedha haujengi utajiri. Katika wiki yake ya kwanza kazini, alikutana na jamii iliyokuwa na njaa na mateso mengi kwa sababu ya umasikini ulio kithiri. Alisikia kuhusu shirika moja lililokuwa na pesa kwa ajili ya umasikini na kisha akaweka mipango na kupata pesa hizo kwa ajili ya jamii iliyokuwa masikini zaidi. Aliridhika.

Lakini hakuwa ameondoa umasikini bali alipunguza makali yake kwa muda tu! Miezi sita baadaye dalili za umasikini zilionekana, jamii haikuwa imesaidika.

Baada ya muda, alihudhuria mafunzo ambapo tofauti hizo mbili zilijadiliwa. Alijifunza jinsi ya kuiongoza jamii kujenga utajiri na kuongeza thamani. Alirudi kijijini na kuwafunza wanajamii jinsi ya kukuza utajiri kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo wakitumia mikopo midogo midogo hivyo basi watakuwa wakuzaji wa utajiri. Jamii ilikuwa na bahati kwa sababu Paul alikuwa tayari kujifunza.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2014.01.22

 Ukurasa wa nyumbani
Kujitayarisha