Ukurasa wa Nyumbani
 Jinsi ya kuanza

Tafsiri:

Bahasa Indonesia
Català
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Română
Српски / Srpski

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

HADITHI YA KWANZA

Hakuiweka njia wazi

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Rebecca alipata kazi nchini mwake, na shirika la kimataifa lisilo la kiserikali. Alipitia mafunzo yao na kuwa na hamu ya kuanza kuiwezesha jamii ya wilaya aliyoisimamia.

Muda mfupi baada ya kuanza, alikumbana na changamoto. Mpangaji wa wilaya alimweleza aandike barua rasmi ya kuomba ruhusa ya kufanya kazi kwenye wilaya hiyo. Aliitwa mbele ya baraza na kuhojiwa kuhusu kiasi cha pesa alichotarajia kuingiza wilayani na miradi atakayo kamilisha. Alikuwa na wakati mgumu kuelezea kwamba hakufahamu kiasi cha pesa wala miradi itakayo kamilika kwa sababu ilitegema vipaumbele vya jamii. Wasiwasi wao ulikuwa kama kizuizi njiani. Alitembelewa na polisi pamoja na maafisa wengine wa kushangaza, wakiuliza kuhusu malengo yake.

Makosa yalikuwa wapi? Hakuchukua muda na juhudi hapo mwanzoni kabla ya kuanza kazi yeyote kwa jamii, kumtembelea mwakilishi wa wilaya na kumweleza jinsi atakavyo nufaika na jamii zilizowezeshwa. Pia, hakuwa amewaonyesha wale wasiotaka mabadiliko,likiwemo baraza la jiji jinsi wangefaidika kwa kuunga mkono mikakati ya kuiwezesha jamii. Changamoto alizokumbana nazo zilisababishwa na mbinu aliyotumia. Kama ilivyo katika mianzo mingi, hata baada ya kugundua makosa yaliyotendeka, ni vigumu kurudi nyuma na kuanza tena.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2014.11.27

 Ukurasa wa nyumbani
Jinsi ya kuanza