Ukurasa wa nyumbani




Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
বাংলা / Baṅla
Български език
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
తెలుగు /Telugu
ไทย / Thai
Tiếng Việt
Türkçe
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

KUDHIBITI MUINGILIANO

Zaidi ya muhudumu mmoja wa jamii

na Phil Bartle, PhD

Imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka


Utangulizi wa kisomo (kitovu)

Nyaraka zinazopatikana hapa Kudhibiti Kisomo

Huwezi kujenga misuli kwa kuinua uzani mara moja

Ukitazama tena maneno muhimu na mawazo yaliyotajwa kwenye Sura ya kwanza na uyaone yenye umuhimu kwako, utakuta neno "Udhibiti." (Halipatikani kwenye kamusi nyingi). Tunawezaje kudhibiti kitu tulichoanzisha ili kiendelee kuwepo?

Kwa jamii, ambayo lengo lao lilikuwa ubora wa afya, na kuchimba choo, swali lao kuu juu ya udhibiti ni, "Tutahakikishaje kuwa choo ,kitawekwa safi, kurekebishwa na kutumiwa?"

Jibu ni kuhakikisha jamii imewajibika (kwa kuhusika kwenye maamuzi na udhibiti) tangu mwanzo wa mradi.

Kwako wewe uliye weka harakati ya mabadiliko, kwa kuipa jamii nguvu,swali kuu juu ya udhibiti ni " Jamii itaendeleaje kushika hatamu za maendeleo yao,kufanya utathmini wa hali yao,kuchagua mambo mapya yanayohitaji kupewa kipaumbele, kutafuta rasilimali zengine, kutenda vitendo vipya, kuongeza uwezo wao wa kujitegemea?"

Malengo yako na ya jamii ni tofauti, lakini yanahusiana.Unataka muingilio wako udhibitiwe. Swali la udhibiti linajibika jinsi unavyoendesha shughuli zako za uchochezi.

Lengo lako sio choo,shule,zahanati au usambazaji maji kwa mara moja pekee. lengo lako ni maendeleo yaliyo dhibitiwa.

Kisomo hiki kinaangazia jinsi unavyoweza kufanya kazi yako idhibitiwe.Sehemu ya jibu, lipo kwenye kurudia mzunguko wa kuiunganisha jamii kufanya jambo; sehemu nyengine ipo kwenye kutambua na kuwafunza wahudumu wa jamii kutoka kwa jamii yenyewe.

––»«––

Kitendo cha manufaa;Utengezaji wa Sabuni


Kitendo cha manufaa

Ukinakili kutoka kwa tovuti hii,tafadhali muungame mwandishi
na uiambatanishe kwa cec.vcn.bc.ca/cmp/

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 12.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani