Ukurasa wa Nyumbani
 Jinsi ya kuanza

Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Română
Српски / Srpski

                                        

Kurasa zengine:

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya tatu

Hakuweza kurudia mzunguko

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Omar alikuwa mhamasishaji mwema. Alifanya kazi na shirika la kimataifa kama mshirikishi wa jamii. Jamii ambamo alifanya kazi ilitaka shule na yeye aliwahimiza na kuwaongoza kupata vifaa, kuweka mipango na kuifuata kwa ukamilifu.

Ujenzi wa shule ulipo kamilika, walifanya sherehe kubwa na kualika wakuu wa serikali, vyombo vya habari na waakilishi wakuu kutoka shirika lake. Baadaye, mwajiri wake alimtuma kwenye sehemu nyengine ya nchi. "Lakini ujenzi wa shule uliwapa ujasiri" Omar alisema "Wako tayari kushughulikia uwepo wa maji safi"

Omar hakuweza kufuatilia maendeleo ya jamii ya kwanza kwa sababu mwajiri wake alimtuma mahali mbali zaidi. Meneja wake hakufahamu kwamba uhamasishaji ni mzunguko unaostahili kurudiwa hadi uweze kujiendeleza wenyewe. Jamii hiyo haikufaulu kujenga usambazaji wa maji safi.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2014.11.27

 Ukurasa wa nyumbani
Jinsi ya kuanza