Tweet Tafsiri:
'العربية / Al-ʿarabīyah |
Hadithi ya TanoHakupeana changamoto kwa jamiina Phil Bartle, PhDimetafsiriwa na Lillian NakaVignetteHadithi fupi zinazoelezea kanuniUamuzi wa Wilson wa kuiachilia jamii kufanya maamuzi yao wenyewe ulipita kiasi. "Jamii inafahamu mahitaji yao," alisema " Tunapaswa kuwasaidia kuyapata mahitaji yao." Alichokosa kutambua ni uwezekano wa jamii kukosa kuyatambua mahitaji yao kwa umakinifu na kufuata maoni ya viongozi wachache waliokosa kuelezea maoni ya jamii kwa ujumla. "Tunahitaji msikiti mpya," walisema katika kijiji cha wakaazi 500 ambacho tayari kilikuwa na misikiti mitano. Wilson pamoja na jamii walitia bidii kufanikisha ujenzi wa msikiti mpya. Kukawa na misikiti mingi zaidi ya watu na rasilimali za kudumisha misikiti iliyokuwepo. Wakati huo huo, watoto wachanga waliangamizwa na ugonjwa wa kipindupindu, wengine wakakosa masomo, barabara za vijijini zikawa hazipitiki na soko likakosa paa la kuzuia mvua. Wilson hakutakikana kuiambia jamii cha kufikiria. Alipaswa kuipa changamoto ya kuchagua walichokihitaji zaidi na jinsi walitaka kutumia rasilimali chache zilizoko kwenye jamii. Iwapo jamii itatetea chaguo lake, basi ingeashiria hitaji la jamii kwa ujumla. Kumbuka:
──»«──Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
|
Ukurasa wa nyumbani |
Jinsi ya kuanza |