Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KIJAMIIKitendo cha uwezeshajina Phil Bartle, PhDimetafsiriwa na Lillian Odembo NakaKifafanuzi cha mafunzoKufuatilia mpango ni kufanyika kwa mradiKatika kipindi cha matayarisho,angalau nyaraka mbili zafaa ziwe zimetayarishwa (na viongozi) na kuidhinishwa (na jamii yote). Nyaraka hizi ni: (1)mpangilio wa utekelezaji wa kijamii, na (2) Mpangilio wa mradi (ambayo yaweza kuwa imetumika katika maombi ya ufadhili). Nyaraka hizi zitasaidia wakati wa ugomvi au utata wa kinachofaa kufanyika, mpaka pale nyaraka hizo zitakapobadilishwa na viongozi na jamii kwa jumla. Ramani ya mradi inafaa iwe sambamba na mpangilio wa utekelezaji kutoka kwa jamii Jukumu lako si kufanya kazi, bali ni kuwezesha jamii kujifanyia mpango huo. Hakikisha watu waliochaguliwa kufanya kazi fulani wanaifanya kazi hiyo. Hakikisha ufuatiliaji wa mradi unafanyika. hakikisha kuna mikutano ya mara kwa mara kwa viongozi (ambapo majadiliano ya maendeleo ya mradi yanafanyika) na mikutano ya jamii kwa ujumla. Hakikisha kumbukumbu sahihi zimehifadhiwa, hasa zile za matumizi ya pesa. Wasaidie viongozi kuweka kumbukumbu ya jinsi wanavyo fanya kazi na mchango wao katika mradi (masaa wanayo tumia katika mikutano, mipango).kumbukumbu zinafaa kuwekwa kuashiria vile masaa hayo yanavyotafsiri kifedha. Hii inamaanisha, mikutano mingi kati yako na viongozi na mikutano michache ya umma na jamii yote. ––»«––Kitendo cha jamii; Kuchimba mtaro: Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mnukuu mwandishi |
Ukurasa wa nyumbani |
Katika utendaji |