Tafsiri:
Kurasa zengine:
|
KATIKA UTENDAJI
Mwelekeo wa jamii
imatafsiriwa na Lillian Odembo Naka
Utangulizi wa kisomo
Nyaraka zinazopatikana hapa Kitendo Kisomo
Mbingu
haitomsaidia asiyetenda. Sophocles
Baada
ya kujitayarisha na kuitayarisha jamii,vitendo vinaanza
Wewe,kama
mhudumu wa jamii hiyo,umekuwa katika hali ya kutenda (wakati wa kuitayarisha jamii)).
Sasa ni wakati wa jamii kuanza kutenda.
Jamii
nzima imechangia katika kufanya maamuzi,imechagua viongozi na kutengeza mpango wao
wa vitendo.Ni wakati wa muondoko.
Kwa
mfano, kitendo kiwe kuchimba choo. Mipango inachunguzwa,vifaa kuletwa,ujenzi unaanza.
Kuna maeneo mengi ambapo wewe kama mhudumu wa jamii unayo kazi ya kufanya.
Jukumu
lako ni kuwezesha mafunzo ya kiujuzi (yaliyo bainishwa na viongozi na jamii wakati
wa ujenzi),hakikisha kazi imefuatiliwa, kwamba kuna maelezo kamili kuhusu shughuli
( hasa matumizi ya pesa) na kwamba jamii haitohisi kwamba mradi huo sio wao.
Kisomo
hiki kinakueleza majukumu yako wakati jamii iko katika hali ya kutenda. Hupaswi kushurutisha
vitendo vyao bali kuwasaidia na kuwapa motisha wa kufanya kazi. Unawapongeza, kuwapa
mawaidha.
Unasaidia
kupata mafunzo yanayo hitajika, kufahamisha jamii,kuweka usawa wa kijinsia,uwazi,
na hadhi kuu ya mradi.
––»«––
Mchango kutoka kwa jamii; Kuleta Vifaa:
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mnukuu mwandishi na uihusishe na cec.vcn.bc.ca/cmp/
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Web Design: Lourdes Sada
––»«––Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011
|