Ukurasa wa Nyumbani
 Jinsi ya kuanza

Translations:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Română
Српски / Srpski

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya pili

Alizidisha matarajio

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Kwame alikuwa na dosari. Alikuwa na majivuno mengi. Alianza kufanya kazi kwenye makazi duni mjini ambapo alifanya mikutano ya kukuza ufahamu kuhusu michakato ya uwezeshaji. Bila kufikiri, aliashiria kwamba angeleta mifereji ya maji katika jamii. Alichomaanisha ni kwamba angeiongoza jamii kuungana na kuleta mabomba yao wenyewe. Aliyasema kwa njia iliyoifanya jamii kudhani kwamba angewaletea mabomba hayo. Hakufanya lolote kuratibisha mawazo ya jamii.

Alipouliza, nani alikuwa tayari kufanya jambo fulani, hakuna aliyekuwa tayari kwa sababu walidhani kwamba Kwame angefanya mambo yote kwa niaba yao. Hawakuwa na muda wa kujiunga na kamati yoyote. Walipogundua kwamba Kwame hangeleta mabomba, walimwita mdanganyifu na mwongo. Hakuweza kufanya uhamasishaji wowote.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2014.11.27

 Ukurasa wa nyumbani
Jinsi ya kuanza