Ukurasa wa Nyumbani
 Jinsi ya kuanza






Tafsiri:

Bahasa Indonesia
Català
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Română

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya Nne

Alidhani kuwa jami ilikuwa imeungana

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Yvette alikuwa akifanya kazi kwenye jamii ndogo ya wavuvi. Alipata wapasha habari wema waliomuarifu kuhusu desturi na wasiwasi uliokuwepo. Aliona kwamba, kilicho hitajika zaidi, ni kiwanda cha kukaushia samaki kitakachotumika na watu wote. Samaki wangekaushwa ili wadumu kwa muda mrefu na kuuzwa maeneo ya mbali. Muda mfupi baadaye, alisikia manung'uniko ya wanajamii kwamba hakuwa na usawa.

Kile ambacho Yvette alikosa kutambua ni kwamba, Jamii ilikuwa imegawanyika na kukosa maelewano. Watu wa makundi mengine tofauti na lile lililompasha habari, walikuwa wakisema kwamba, wanawake walikuwa na viwanda vya kibinafsi vya kukaushia samaki na wangehitaji zaidi soko la kuuzia lililofunikwa.

Hakuweza kupata makubaliano ya ujumla kwa sababu ya mgawanyiko wa wanajamii na alionekana kupendelea upande mmoja na kukosa kuweka usawa. Ingawaje jambo hilo lilieleweka baadaye, meneja wake alimtuma kwenye jamii nyengine na kuleta mhudumu mwengine ambaye hakufahamika na jamii ya wavuvi.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2015.01.14

 Ukurasa wa nyumbani
Jinsi ya kuanza