Tweet Tafsiri:
Català |
UHIFADHI WA UTAMADUNIMwandishi Phil Bartle, PhDMwanaharakati na MsomiTuzo kwa Audra TailleferKwa hivyo unataka kuihifadhi utamaduni wako. Kipeo kizuri. Lakini, waweza kushangaa ukigundua kwamba wewe ni tisho kwa utamaduni wako ukitaka kuihifadhi. Hiyo ni kinaa kweli? Si kinaa, unapochunguza kwa maakini maana ya utamaduni, na vile unavyoweza kuiimarisha. Utaratibu wa uwezo wa tovuti hii una utovu kwenye kuiimarisha, wala sio kuihifadhi. Unataka kuiwezesha ama kuihifadhi utamaduni wako? Uamuzi ni wako. Chagua moja tu. Hauwezi kuchagua zote mbili. Sifa za Utamaduni: Kabla ya kujadili uhifadhi wa utamaduni, tunafaa kukubaliana juu ya maana ya utamaduni. Kimsingi, ufafanuzi wa utamaduni ni kwamba imebuniwa na mafunzo yetu yote. Makala kadhaa ya mafunzo kwenye tovuti hii yanajadili utamaduni. Baadhi yao ni: Utamaduni na Ufafanuzi wa jamii. Zote zinasisitiza kwamba utamaduni ni mfumo wa ushirika ama kijamii, kwamba ni itikadi zetu zote na matendo ambayo hairithishwi na majeni. Huwekwa na kurithishwa na viashirio. Hushirikishwa na vipimo sita vya: kiteknolojia, kiuchumi, kisiasa na kitaasisi, na kipimo cha utamaduni cha haiba na karama, na maoni yetu ya kidunia, ama asili ya ulimwengu. Ufafanuzi wa utamaduni wa kimtaa ni ambayo sisi katika sayansi za kiushirika huona kama moja ya vipimo sita, uhaiba. Upigaji ngoma na uchezaji wa densi Afrika, upigaji ngoma na wimbaji, mashinani, Marekani Kaskazini, densi ya ''ballet'' na usanii wa opera Ulaya, yote haya ni baadhi ya utamaduni lakini si utamaduni kwa ujumla. Kwa maana hizo wimbo, densi na muziki za kiutamaduni ni elementi muhimu katika utambulisho wa wale wanao zitimiliza na kuzitafaraji, tunaunga mkono kwa uthabiti wazo la kuzihifadhi na kuziongeza, na kuongeza umaarufu wao katika jamii zote. Hisia thabiti ya utambulisho ni elementi ya thamani katika uimarishaji wa jamii na utamaduni wao. Tazama Elementi za Uwezo. Ni kwenye vipimo vingine na vipengele vya vipimo hivyo, ambamo uhifadhi wa utamaduni unaweza kusababisha madhara kwa uimarishaji wa utamaduni huo. Vipengele vya Uhifadhi: Tafakari kuhusu vitu tunavyojua huihifadhiwa: achali ndani ya chupa ya kuhifadhi, vipepeo ndani ya kasha ya kioo, ngozi kwenye pochi, mraba ndani ya chupa ya kuhifadhi, miriti za ujenzi, wadudu kwenye kaharabu, vyura kwenye gesi ya kuhifadhi. Vyote vina ushiriki mmoja, vyote vilikua hai wakati moja (ama vilikua sehemu ya vitu hai) na sasa vyote vimekufa. Harakati ya uhifadhi ni ile ambayo hugeuza kitu ili kidumu, ili kisigeuke, ili kisiwe na uhai. Kua hai unahitaji kitu kiwe na mwendo, mageuzi. Kwa hivyo ukitaka kuhifadhi kitu, unafaa kukiua. Mwishowe kitabadili bila kujali kilivyohifadhiwa. Wacha Utamaduni Usitawi na Uwe Thabiti: Ukirejea makala ya utamaduni; utapata utamaduni una uhai. Umeundwa kutokana na viashirio, nuio na tabia ya wanaadamu, lakini yaweza kuishi kupita miaka ya wanaadamu wanayoimiliki. Ni kama kidubini, ijapokuwa hauna ubiolojia. umepita yale ya kiubiolojia. Siwezi kupa uhuru. Kama uhuru unaweza kupeanwa, unaweza kuzuiwa (kulingana na mafunzo ya Lao Tsu) na basi hautakua uhuru wa kweli. Mafunzo ya uwezo kwenye tovuti hii yamelengwa kwa kupambana na umaskini na unyanyasaji, wala si maskini na walio nyanyaswa. Mbinu hii inalenga kuimarisha jamii za watu maskini na walio nyanyaswa. Ili hizo jamii ziwe imara, lazima zibadilike, kwa hivyo utamaduni wao lazima ubadili. Lazima zitekeleze mambo haya zenyewe; tunaweza tu kuongoza na kusisimua. Kwa maana utamaduni ni yote wanaadamu hujifunza, mageuzi yanayotakikana ili iwe imara zaidi yanahitaji utamaduni ubadilike. Maendeleo ni mabadiliko (vilevile wozo). Wacha zisitawi. Ua litakua likipata maji yakutosha, mwangaza,udongo na mbolea. Halitarefuka ukilingoa kwa ujuu. Tunaweza kulipatia maji na mbolea, lakini lazima liendelee lenyewe (kama jamii maskini). Kulingoa kwa ujuu ni kama uhandisi wa ushirika. Kulisisimua kwa kulipa maji na mbolea ili likue na liwe imara ni utaratibu wa uwezo wa mauua. Watu wengi wanaamini hadithi za kale ambamo utamaduni wa kiasili ulikua timamu. Ushuhuda ulioko ni tofauti. ''Siku barabara za kale'' hazikuwa. Hakuna jamii yoyote ya ukoloni iliepuka kubadilika. Kulikua na fujo, kulikua na vita, kulikua na mambo hayakua ya haki, kulikua na mabadiliko na marekebisho. Hatufai kuamini kwa kale isiyo ya kweli na kuhifadhi kitu hakikuwa. Hapo na sasa, ushupavu, maendeleo na ustahimili ulihitaji na unahitaji mageuzi na ujasiri. Teua na Chagua: Tumenena ya kwamba tunahimiza uhifadhi wa nyimbo, densi na muziki, kwa sababu zinakoleza hisia ya nafsi, sehemu muhimu ya maendeleo ya uwezo. Lakini tunafikiri kwamba kuna haja ya baadhi ya itikadi kubadili kama jamii itaimarika. Kwa nukta moja tafakari utamaduni ni kama mavazi. Kwa hakika, mavazi ni teknolojia, sehemu ya utamaduni wetu. Tunavaa mavazi tofauti kulingana na hali za anga. Hatuwezi kuwinda sili barafuni uchi, na hatuvai nguo nzito tukienda kuogelea baharini. Ili kuendelea na kubadili kwenye hali zinazogeuka, lazima tuwe na uwezo wa kuvaa vipengele tofauti vya utamaduni wetu katika hali tofauti. Fumbo lingine: tafakari utamaduni ni kama njia yetu ya usafiri. (Njia yetu ya usafiri ni kipengele kingine cha uteknolojia cha utamaduni wetu). Hatuendeshi gari jikubwa kwenye bahari kuvua samaki. Hatuendi kwa mashua ya uvuvi kuwinda twiga katika Jangwa la Kalahari. Twateuwa na kuchagua kile laiki na chenye manufaa. Kama uhai wetu, maendeleo na ushindi wetu unazuiwa kwenye mazingira tunayoishi na baadhi ya vipengele vya utamaduni wetu, basi tunafaa kumiliki sifa mpya za kiutamaduni. Tazama makala juu ya Utohara wa Wanawake. Baadhi ya hizo sifa za kiutamaduni nizaheshima na sifa sana, lakini zikitufanya tuwe wanyonge na tufifie, zinafaa kubadilishwa kama mavazi mapya ama namna mpya ya usafiri. Tukisema, ''hatushtakiani na kupigana,'' na tujivune kuhusu kipengele hicho cha utamaduni wetu, basi tutapoteza haki yetu wakati wa kupigania haki yetu ukifika, na tukose kupigana. Tukisema, ''sisi huwaheshimu na kutii waliomamlakani,'' na kama waliomamlakani ni wafisadi na waovu, basi, kwa muda, lazima tuweke kando hiyo sifa ya kiutamaduni ama tumiliki seti ya sifa yenye manufaa zaidi. Kama hatuwezi kufanya hivyo, basi tutanyanyaswa, tuibiwe, na tudhulumiwe na viongozi wetu. Kwa hivyo, hatufai kusema ati lazima tuchague sehemu bora kabisa ya utamaduni wetu wa kiasili na tuihifadhi. Tunafaa kusema lazima tuthibitishe unafsi wetu, na tuwe na uwezo wa kubadili itikadi zetu, tabia zetu, mafikira yetu, tutumie zile zitakazo tufanya tuwe bora zaidi (sio zile zitatufanya tuwe na heshima lakini wanyonge). Ingawaje mavazi ya ''parka'' yana heshima, hayatakua na manufaa kwetu tukiogelea baharini. Afrika ya kisasa na Marekani ya Kilatini, jamii za Ulaya za mashinani, nchi maskini, zote ambazo zinaishi kwenye mazingira yanayohitaji mageuzi katika baadhi ya sifa za kiutamaduni. Tunafaa tuchague zile ambazo zitatuimarisha, kwa uwezo wetu wenyewe. Kimalizio; Kwa hivyo unataka kuihifadhi utamaduni wako? Kwa mafunzo ya uwezo kwenye tovuti hii, tunasisitiza kwamba kuhimiza ushiriki na utoaji wa uamuzi wa jamii haimaanishi kukubali kwa utiifu maombi yote ya jamii. Inamaanisha kupingana na kuhimiza jamii kufafanua na kuchunguza kwa maakini kile wanachotaka na wanachotaka kutimiza. Mwishowe lazima watekeleze wajibu wao. Baadhi y changamoto kama mwanaharakati ni kufahamu maana ya mambo haya, matokeo na manufaa yake. (Ndio kwa maana tunawakifu upungufu wa umaskini na kulenga maondoleo ya umaskini). Wazo la ''Uhifadhi wa Utamaduni'' lisipochunguzwa, lina hisia ya kupotosha. Mwanzoni, tunadhani tunaweza kuiunga mkono. Lakini, ukaguzi wa maakini utadhihirisha ya kwamba ni kwa kweli kinyume cha kile tunachotaka. ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Sahifa Kuu |
Uwezo wa Jamii |