Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
SHEREHEMwisho na Mwanzo mpyana Phil Bartle, PhDimetafsiriwa na Lillian Odembo NakaKifafanuzi cha MafunzoSherehe sio likizo bali ni sehemu muhimu katika utenda kaziUpangaji na Utekelezaji wa sherehe za kijamii ni kazi ngumu na muhimu katika kuileta jamii pamoja. Pengine hujagundua kuwa; kwa wanafunzi na wafanya kazi wengi, sherehe ni mapumziko kutoka kwa masomo au kazi. Lakini kwako wewe, sherehe ni moja kati ya majukumu yako. Kama ilivyo dhahiri wakati wa kusherekea (yaani kumalizika kwa mradi),unapaswa kuhimiza shere zengine katika harakati: kuchangisha pesa, kuweka jiwe la msingi, kupeana cheki, Kumalizika kwa awamu muhimu ( Ukuta, paa, upakaji rangi) na sehemu zingine. Kupiga ngoma, kudensi, mchezo wa kuigiza, maonyesho ya vipawa na aina zengine za tamasha vyafaa kujumuishwa kwenye kila sherehe. Yaalike makundi ya tamasha kutoka kwenye jamii na shule ili kutumbuiza. Hakikisha watu wenye hadhi kuu wamehudhuria na kutoa hotuba za kuisifu jamii (wala si kugeuza sherehe kuwa kongamano la kisiasa) pia yaalike mashirika ya utangazaji na wanahabari. Kwa nini? Sherehe hizo huongeza hamasisho kwa jamii na umma na kulipa nguvu jukumu la ustawishaji wa jamii wala si mradi huo pekeyake Ni pahali pema pa hamasisho, kuboresha uwazi na kuweka mradi wa kijamii kuwa kitendo chenye hadhi kuu. Unapaswa kupanga mipango yote pamoja na viongozi wala si kuwafanyia kila kitu. Himiza, sifu na uwape wasia,- kwamba wanaweza, Tazama "Sherehe." Burudika. ––»«––Kumalizika kwa mradi;Sherehe na maadhimisho: © Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Ukurasa wa nyumbani |
Katika Utendajji |