Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
RASILIMALI ZA NJEKuweka Uwiano kati ya Rasilimali za Ndani na Njena Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Elie ChansaKitini cha MafunzoMsaada kiasi gani unaweza kuja kutoka nje ya jumuiya kabla jumuiya haijawa tegemezi kwa msaada wa nje, na hivyo kupoteza uwajibikaji binafsi?Kama mratibu, utaona kuwa ni vigumu kuwa na uwiano kati ya rasilimali zitokazo nje ya jumuiya, na zile za ndani. Wewe na viongozi wa jumuiya mtakuwa katika presha kubwa tu, ili kuleta rasilimali za nje kwenye jumuiya. Mashirika wafadhili wanataka kusaidia wakati wanajumuiya wanataka kupokea. Unafamu hata hivyo, kuleta rasilimali za nje kunachangia gonjwa la utegemezi na kupunguza uwezo wa ustahimilivu na kujitegemea. Licha ya hivyo, kuna njia za kuongeza uwezo wa kutumia rasilimali za nje, kama ilivyooneshwa kwenye hadithi ya Mohammed na kamba. (Tazama Kuhadithia). Kama unaweza kushawishi wafadhili wa nje kugharamia mafunzo ya maarifa, mafunzo ya uongozi, na uratibu, na kuwezesha jumuiya kupata rasilimali ujenzi kadhaa za kwao, utaweza kuchangia kwenye kujitegemea na ustahimilivu. Kama Mtume, amani iwe juu yake, angempa chakula ombaomba, angekuwa anamfudisha ombaomba kuwa ombaomba; kwa kumpa ushauri na mtaji badala yake, alimsaidia ombaomba kuwa mwenye kujitegemea. Mtandao huu unakusaidia kupata rasilimali za nje, kama kwenye Michanganuo, itakayokusaidia kuandaa michanganuo yenye nguvu. Kama chombo chochote chenye nguvu (kwa mfano, moto), maarifa haya yanaweza yasitumiwe ipasavyo na yanaweza kuchangia kwenye umaskini kwa mtazamo wa muda mrefu. Yatumie vizuri, kwa ajili ya mwisho sahihi. ──»«──© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Ukurasa wa nyumbani |
Matayarisho |