Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
KUPANGA UMOJAIlete Jumuia yote PamojaNa Phil Bartle, PhDimetafsiriwa na Jacob LisakafuTraining HandoutKwa hali ya "kawaida" kila jumuia ina aina mbali mbali za utengano wa kijamiiUmeona mwanzo lazima uwakikishe wanawake wanaudhuria mikutano ya jamii unayoitisha (isipokuwa:Jumuia zisizopenda mabadiliko za kislamu). Pia : walemavu, vijana, wazee, watu dhahifu, wenye tabia mbaya,watu waliotengwa, wanaoona haya na wastahafu. Hii ni sehemu ya mikakati yako ya kuiunganisha jamuia. Angalia Kupanga umoja. Kila jamuia inamvutano wa kuvuta kuelekea nje. Hii inatokana na tofauti katika ukoo, ukabila, dini, matabaka, jinsia, umri,elimu, nguvu na uwezo wa akili, hajira,kipato, utajiri, umiliki wa ardhi (mwenye ardhi, mpangaji, mvamizi wa ardhi na wengineo) na mambo mengine ambayo yanaganwanya wananchi. Angalia Kutengana kwa Jamii. Ni muhimu kama muamashishaji, utaangaliwa kama haupo upande wowote. (Kama refa), haupo upande wowote au kupendelea upande wowote. Hii maana yake ni lazima Uijue jumuia kiundani zaidi. Kama utatumia muda mwingi na baadhi ya watu, watu wengine watafikiria unapendelea upande mmoja. Usiogope kwenye watu wengi kuchangua vikundi tofauti katika jamii, lakini kwa haraka lazima usema haupendelei upande wowote au kikundi chochote. Kumbuka, tena,hauna lengo la kuweka jumuia ifanane (wote kuwa pamoja), lakini ni umoja wa jumuia maana yake vikundi vyote vina nafasi sawa kwa jamii zote na katika mazingira ya kuvumiliana, watu wote waelewane na kuheshimiana kila mmoja,kwa kidini,matabaka, ukoo, jinsia, uwezo,makabila, lugha, au umri. Kuinganisha jumuia ni mwanzo wa kuitambua jumuia moja matatizo yao ya msingi na malengo yao. ––»«––Uchangiaji wa jumuia: Ukiiga kutoka kwa tovuti hii, tafadhali muungame mwandishi) |
Ukurasa wa nyumbani |
Tuanze mada |