Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
IJUE JAMII UNAYOLENGANani Afaidikaye Tokana Vitendo Vyako?na Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Marcellus CheggeVitoleo vya mafunzoKuwa mtafiti wa jamii na mchanganuzi; Mfinyanzi shupavu lazima ajue sifa bainifu ya udondoMethali nyingine itumikayo katika uwezeshaji wa jamii ni “Mfinyanzi lazima aujue udongo wake.” Udongo wako ni jamii. Unataka kuifinyanza, uiendeleze ipate nguvu. Ili ufaulu kufanya hivyo lazima ujue na kuifahamu vyema hiyo jamii (na pia ujue na kufahamu hali ya jamii kijumla). Lazima ujue mengi iwezekanavyo kuhusu mpangilio wa hiyo jamii, uchumi wake, lugha zake, matatizo yake, siasa zake, ramani zale na ikolojia yake. Utafiti wako usiwe tu hutafuta orotha ya mambo ambayo hayahusiani; utahitaji kuyachanganuza hadi uelewe kina cha jamii hama mfumo wa ujamaa. Waza kuhusu jinsi elementi tofauti zinahusiana. (Tazama “Jamii ni nini?” Na “Utafiti wa Jamii”). Mwanzo mzuri ni kuchora ramani (map). Watu wanaishi wapi? Kuna huduma gain kati ya hiyo jamii? (kama barabara, vichochoro, mitambo ya maji, kliniki, shule, usafi afya, soko na huduma zinginezo). Baadaye, utakopo waongoza (assessment) wana jamii kwa ukadiriaji wa wa hali yao (rasilimali, mahitaji, mafaa na shida), utawaongoza kuchora ramani ya kijamii. Ukichora yako binafsi sasa, utasaidika kwa matayarisho ya hiyo ramani ya pamoja baadaye. Andika muhtasari wako kwenye shajara. Eleza maoni yako kuhusu: mpangilio wa jamii, uchumi, lugha, siasa, thamana za mgao, tamaduni, na uhusiano wao wa kimaumbile na mazingira (ikolojia). Endelea kuchanganuza jinsi elementi tofauti zinahusiana. Utajifunza ya kwamba jamii sio tu mkusanyiko wa watu binafsi lakini ni mfumo unaopita mipaka ya hao watu binafsi. Kama mfumo jamii ina vipimo kadhaa, vya kiteknolojia, via kiuchumi, vya kisiasa, via jingo la ustawi wa jamii, via itikadi na kimawazo, Watu huja na kuondoka katika jamii, kwa kuzaliwa, kifo na uhamiaji, na hata hivyo mfumo unashikilia. Huu mfumo hubadilika kila wakati. Kazi yako ni kuelewa huu mfumo ili uweze kuashiria kwa kudukua (nudge) hayo mabadiliko na kuyaelekeza upande fulani (kama ilivyoelezwa kwenye vikomo vyako ambavyo tulivijadili awali). Kuna chungu nzima ya kujifunza kuhusu jamii unayolenga na haifai kukomesha hayo mafunzo. ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Ukurasa wa nyumbani |
Matayarisho |