MAHITAJI YALIYOZALISHWA NA JAMII
Wala si mahitaji yaliyozalishwa na Shirika
imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka
Kifafanuzi cha mafunzo
Mradi uanzapo,viongozi wanafahamu zaidi ujuzi unaohitajika
mradi unapoendelea, viongozi na jamii watagundua kwamba wanahitaji ujuzi mpya.
Ujuzi
huo waweza kuwa uchoraji,useremala, ujenzi na ujuzi mwingine unaoambatana na ujenzi.
Ujuzi zaidi waweza kuwa wa kifedha, kupanga mipango, kuweka kumbukumbu, kuchangisha
pesa, kuandika ripoti, kusuluhisha ugomvi na kudhibiti miradi.
Mafunzo
yaweza kuwa ya papo hapo kwenye mradi ambapo yule anayefahamu ujuzi fulani ana wafunza
wasio jua au yale ya kuhudhuria masomo shuleni aidha zile za serikali au za kibinafsi.
Unapaswa
kusisitiza mafunzo ya papohapo kwenye mradi kwa kutumia rasilimali zipatikanazo katika
jamii hiyo. Wazee katika jamii hiyo, walio na ujuzi wanaweza kuwafundisha vijana.
Ikiwa
Ujuzi unahitajika kukodiwa, ni vyema kukodi kutoka kwa jamii yenyewe na ujumuishe
mafunzo ya wale wasioufahamu ujuzi huo (wake kwa waume).Hakikisha viongozi wanaweka
kumbukumbu ya mafunzo yeyote ya papohapo kwenye mradi.
Kama
mafunzo ya papohapo hayawezekani, waweza taja uwezekano wa mafunzo ya shuleni. Lazima
kuwe na bajeti, mahali pesa zitatoka ili kulipia masomo hayo.
Kama
makadirio hayo ya mafunzo yatafanywa mapema , yanaweza kujumuishwa kwenye maombi
ya ufadhili Kutayarisha
warsha.
Kulingana
na bajeti, watu zaidi waweza kupelekwa kwenye mafunzo hayo ya shuleni.
Jukumu
lako ni kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yameidhinishwa na jamii yote, na yana umuhimu
katika mradi wala sio tu kumnufaisha mtu mmoja.Pia hakikisha wale watakaohudhuria
mafunzo hayo wamechaguliwa na jamii yote ili kuzuia tashwishi za upendeleo.
Ikiwa
mafunzo yatahitajika wakati mradi unapoendelea, hakikisha wanaohudhuria wameidhinishwa
na jamii yote, ufuatiliaji na rekodi kuhusu masomo yao iwekwe na ijumuishwe kwenye
ripoti ya maendeleo.
––»«––
Mkutano wa jamii; Kutathmini mahitaji
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Web Design: Lourdes Sada
––»«––Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011
|