Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
NGUVU KWA KUPITIA MAFUNZO YA UONGOZIKushirikisha Kila Mtu katika Uongozina Phil Bartle, PhDimetafsiriwa na Angelica Mulokozi ChristinKwa Kumkumbuka Gert LüdekingUtangulizi wa KijenziNyaraka Zilizoambatanishwa katika Mafunzo ya Uongozi ya Kijenzi Hiki
Uongozi ni wa muhimu sana hivyo hauwezi kuachiliwa kwa wakurugenzi tuMafunzo ya Uongozi, kama yalivyoelezewa kwenye tovuti hii, yana namna maalum ya utendaji. Ni kitu ambacho kinazidi mafunzo ya kawaida, na ni kitu ambacho kinaongeza, kwa njia ya moja kwa moja, uwezo, nguvu na kuwezesha makundi, mashirika au jamii kumudu. Utaona kuna kuingiliana kwa kiasi fulani kwa kijenzi hiki na vijenzi vingine. Kwa mfano, mpango wa uhamasishaji wa jamii umechanganyikana kwa kiasi kikubwa na mpago wa mafunzo ya uongozi (unaohusiana na jamii), kwahiyo mipaka kati ya mipango hii miwili sio rahisi kuitambua. Hapa utakuta baadhi ya nyaraka katika kijenzi hiki. Maswali Manne ya Msingi ni orodha ya maswali manne ambayo ndiyo msingi wa mafunzo ya uongozi. Pamoja, maswali haya na majibu yake, ujenga hoja yenye mantiki, ambayo ndiyo shina la muundo wa mradi na mambo mengine yote yanayohusika na uongozi. Mafunzo ya Uongozi ni karatasi ya mazoezi ya semina kwa washiriki ambayo ina orodhesha tena maswali manne, na baadhi ya kanuni nyingine za maamuzi ya uongozi. Tazama pia Mafunzo ya Uongozi ya sura ya tatu ya "nguvu kwa kupitia kwenye mafunzo", ambayo ni mtaala wa mpango wa mafunzo ya jamii. Mafunzo ya Uongozi, Maelezo kwa Mwalimu, yanahusu wasaidizi au walimu, na yanaelezea namna ya kutumia nyenzo na kufanfanua kanuni za mafunzo ya uongozi, Muhtasari wa Mkakati wa Mafunzo ya Uongozi , ni muhtasari wa mkakati wa MMJ (Mpango wa Mafunzo ya Jamii), na unaonyesha namna mafunzo ya uongozi ni mojawapo ya misongamano mitatu ya kwenda mbele ya utendaji inayolenga kuongeza uwezo wa kumudu wa jamii za vima vya chini. Mfafanuo wa Mkakati wa Mafunzo ya Uongozi , ni upanuzi wa muhtasari, lakini unaotazama kwa undani zaidi kila kipengele kilichoko katika mkakati. Kujiandaa kwa Mafunzo, kunaeleza namna ambayo mafunzo, katika mpango huu, yanapita fikira za kawaida za kwamba ni ugawaji wa ujuzi, na yanaweza kutumika katika urekebishaji wa taasisi (upangaji upya wa kundi, shirika au jamii ili iendeshe shughuli zake vema zaidi na iwe na uwezo mkubwa zaidi).
Vijenzi visaidizi Uongozi kwa Kushirikiana, Kuwezesha Uhamasishaji
––»«––Mafunzo ya Uongozi: (Kama
ukinakili maandishi kutoka kwenye tovuti hii, tafadhali onyesha majina ya waandishi) |
Ukurasa mkuu |