Fasiri
Kurasa nyingine:
|
KUWA MHAMASHISHAJI
imetafsiriwa na Wamalwa Philip
Kijitabu cha Mafunzo
Je umejiandaa kuwa mhamashishaji, mwelekezi au mwanaharakati?
Kujijaribu:
Kadiria ujuzi na maarifa uliyo nayo. Jiulize:
- "Je
nikotayari kupeana muda wangu na kuacha shughuli zangu ili kuwasaidia watu katika
jamii kujitatulia matatizo yao wenyewe?"
- "Je
nina mienendo na tabia ambayo watu hawatanichukulia kama ambaye anajivuna?"
- "Je
ninaweza kufanya kazi katika jamii fulani bila kujiingiza kwenye siasa, migawanyiko
na migogoro ilioko kwenye jamii hiyo?"
- "Je
ninaweza kudumisha matakwa na hamu ya watu wa jamii ninayoitumikia?"
- "Je
niko tayari kufanya kazi kwa namna ambayo watu wa jamii ninayoitumikia watahisi kuwa
walijifanyia mambo wenyewe wala hawakufanyiwa?"
- "Je
nina ujuzi wa kutosha wa kimsingi katika mambo ya ukulima, teknolojia inayofaa, ujenzi,
mambo ya ulemavu, ujenzi wa barabara, lishe, kazi ya jamii, kuhifadhi ardhi, usafi
na maji; ili kuwasaidia watu katika jamii kutambua na kutatua shida zao wenyewe?"
- "Je
niko tayari kuepuka kuvujwa moyo wakati mambo yanapokwenda kinyume na nilivyotarajia
au kukusudia?"
Ikiwa
unavipaji hivi, basi utakuwa tayari zaidi kuwa mhamashishaji mwenye mafanikio.
Jukumu
la Mhamashishaji:
Jukumu
la mhamashishaji ni kuhamashisha jamii ili ikumbatie miradi itakayopelekea jamii
hiyo kuongeza uwezo wake na kujitegemea. Haswa,
hiyo inajumulisha yafuatayo:
- Kuita
mikutano ya jamii ili:
- kuwajulisha
wanachama wa jamii yote juu ya habari sahihi kuhusu jinsi jamii hiyo inaweza kujitegemea;
na
- kuandaa
na kutafuta rasilimali na vifaa vyote (vya kibinadamu na mali) vinavyohitajika kwa
shughuli za miradi ya jamii;
- Kusisimua
watu katika jamii kushiriki katika miradi ya maendeleo ya jamii yao;
- Kushiriki
katika miradi ambayo itakuza ufanisi na uwezo wa jamii na kujitegemea;
- Kuhakikisha
kuwa habari zote ni sahihi na kwamba zimeeleweka vizuri;
- Kukabiliana
kwa dhati na habari za uwongo au sisizo sahihi, haswa zile zinazosababisha matarajio
yasio na msingi au yaliopindukia, na ambayo hatimaye hufanya watu kuvunjika moyo;
- Kuwatia
moyo na kuwapongeza wana jamii, na kuwahakikishia kuwa wana uwezo wa kujiendeleza
wenyewe;
- Kuhakikisha
kwamba maamuzi yote kuhusu miradi ambayo jamii itaanzisha ni chaguo la jamii yote
na wala sio tu viongozi wa jamii wachache (wenye nguvu);
- Kuhakikisha
kwamba watu waliobaguliwa au wenye uwezo mdogo katika jamii wamesikizwa na kutiliwa
maanani kwenye maamuzi ya jamii: wakiwemo wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, kabila
la watu wachache, wanyonge na walionyimwa haki za uraia au ya kupiga kura;
- Kuendeleza
na kukuza umoja katika jamii, umoja wa nia maalum, umoja wa malengo na vitendo; na
kukumbana kwa dhati na nguvu zinazochochea katika jamii migawanyiko, hisia za chuki,
itikadi mbovu, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa jinsia, ukabila, mapendeleo ya kiukoo
na tabaka;
- Kukutana
mara kwa mara na wahamashishaji wengine ili kubadilishana ujuzi na uzoevu, kutatua
matatizo yanayofanana pamaja na kuimarisha ujuzi wa kusisimua jamii na uongozi wa
jamii.
- Kuwasaidia
viongozi na wanachama wa jamii kujifunza ujuzi na maarifa ya uongozi wa jamii.
Mhamashishaji wa
jamii ni yule ambaye anasisimua jamii,
na anatakiwa kuwa na maarifa na ujuzi kuhusu kanuni muhimu ya kuhamashisha jamii,
na mwenye kiu ya kujifunza zaidi jinsi jamii zinaweza kusisimuliwa ili kuleta umoja
na utangamano, kuzisaidia jamii kufanya maamuzi yake yenyewe, kujipangia miradi,
kutambua na kutoa rasilimali yake kwa miradi hiyo, na kuchaguwa mikakati inayofaa
zaidi kwa kutumia rasilimali za ndani na nje ili kufikia malengo ya jamii. Tazama: Majukumu
ya Mhamashishaji.
––»«––
Mhamashishaji Kazini:
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Web Design: Lourdes Sada
––»«––Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011
|