Ukurasa wa nyumbani
 Changia mawazo




Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / Hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
한국어 / Hangugeo
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
Tiếng Việt
Türkçe

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

DONDOO ZA UCHANGIAJI MAWAZO KWA WASHIRIKI

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka


Kifafanuzi cha mafunzo

Msahalishi aweza kuzisoma dondoo hizo kwa sauti.Zaweza kupewa washiriki ili wajisomee kabla ya kikao

Kanuni za mchezo:

"kikao cha kuchangia mawazo" ni kama mchezo.Sio mchezo wa mashindano ambapo mshiriki angependa kushinda.Ni mchezo wa kushirikiana ili kundi lote lipate ushindi.

Kama ilivyo, kwenye mchezo wowote kuna kanuni.Kanuni hizo ni bandia na za muda.Kwa mfano, kanuni katika mchezo wa kandanda zinahitaji mpira usalie ndani ya kiwanja.(mpira ukitoka nje ya kiwanja, itabidi mchezo usimamishwe hadi mpira utakaporudishwa kiwanjani,).Kanuni za mchezo wa kandanda sio kanuni za maisha na hutumika wakati wa mchezo huo pekee.

Ili kikao cha kuchangia mawazo kifikie malengo yake, ni muhimu kwa mshiriki kufahamu na kutekeleza mchezo unavyostahili. Kanuni za kikao cha kuchangia mawazo ni chache na rahisi. Wakati mwengine zaweza kusahaulika kwenye furaha ya mchezo.Ni jukumu la msahalishi kuwakumbusha washiriki juu ya kanuni hizo wanapozisahau.

Kanuni moja ya msingi kwenye kikao cha kuchangia mawazo ni kwamba msahalishi ndiye anayeuliza maswali. Maswali hayo yanakusudiwa kukuongoza wewe na washiriki wengine kwenye kikao hicho. Wewe pamoja na washiriki wenzako mwapaswa kuchagua majibu kwa pamoja (hii itapelekea uamuzi wa kundi wala si uamuzi wa mtu). Jukumu la msahalishi kwa kuuliza maswali ni kutilia maanani mada ya siku na pia kusaidia katika harakati ya maamuzi ya kundi.

Kanuni muhimu kwenye kikao hicho ni kwamba kusiwe na majibizano wala misuto. Msahalishi anapouliza swali, kila mshiriki amealikwa kuchangia.Mshiriki yeyote anapochangia,hakuna mshiriki mwengine anayestahili kuongea kuhusu mchango huo. Kumbuka kwamba kanuni hii itatumika wakati wa kikao cha kuchangia mawazo na wala si katika hali ya maisha.(hatufuati kanuni za kandanda nje ya uwanja kwenye hali ya maisha).Tambua kuwa msahalishi pia hafai kuongea kuhusu mchango uliotolewa na mshiriki.Yeye ataandika vidokezo vyote ubaoni.

Kanuni hii ni muhimu. Ukidhani kuwa dokezo kutoka kwa mshiriki si sawa, kuwa na subiri,usiongee kulihusu dokezo hilo wala kulikosoa. Hata hivyo unapaswa kutoa vidokezo hata kama haviambatani na vingine na msahalishi ataandika vidokezo vyako ubaoni.

Jukumu la msahalishi wako ni kukiongoza kikao .Waweza kushawishika kuongea kuhusu vidokezo vilivyotolewa au hata kuvikosoa.Jipe nidhamu na uhutubie kundi zima kuhusu vidokezo vyako kupitia kwa msahalishi.Hii italisaidia kundi na kuwezesha kikao kufaulu kufanya uamuzi wa kundi.

Mada:

Mbinu za kuchangia mawazo zaweza kuundwa upya na kutumika katika hali na mada tofauti. Azimio kuu kwenye mfuatano huu wa kisomo cha usimamizi wa jamii ni kujenga uwezo na kuwezesha jamii. Kwa hivyo mada zitakazolengwa na msahalishi wako zitahusiana na azimio hilo.

Msahalishi ataanza kwa kuuliza matatizo ya kundi (au jamii). Utaalikwa pamoja na washiriki wenzako kutoa vidokezo, kisha msahalishi ataviandika ubaoni.Lapaswa kuwa swali nyeti kwa kundi (au jamii).

Pengine ungependelea kutoa pendekezo kuwa; shida kubwa katika jamii ni kwamba hakuna ukumbi wa kucheza dansi.Msahalishi hatakubali au kutokubaliana nawe;ataliandika pendekezo lako ubaoni.Watu wengine waweza kutaka kukukosoa, lakini hakuna muda wa majibizano kwenye kikao cha kuchangia mawazo.Washiriki wengine waweza pendekeza kuwa, hakuna usafiri wa kutosha, wengine waseme hakuna maji safi ya kutosha, wengine waseme magonjwa yamezidi au hali ya umaskini imekithiri.Msahalishi hatalihukumu pendekezo lolote.Kundi zima,wala sio mtu mmoja au sehemu ya kundi, lina jukumu la kufanya uamuzi kwa usaidizi wa msahalishi.

Kundi likizipa shida zao kipaumbele (yaani kuziorodhesha kulingana na umuhimu wake kwa kundi hilo),Msahalishi atawaelezea kwamba lengo la kwanza ni kwa kundi kutatua shida iliyopewa kipaumbele.

Lengo, ni kitu cha ujumla kinacho tumainiwa.Sio mahsusi na hakiwezi kukadiriwa.Jukumu litakalofuata kwa msahalishi ni kulisaidia kundi kutafsiri lengo hilo la jumla liwe mahsusi na la kukadiriwa.(Tazama kifafanuzi HODARI kwa orodha ya sifa za malengo).Kipengele hiki kwenye uchangiaji mawazo ni mahsusi kwa udhibiti wa mafunzo kwa jamii na hakitumiki katika aina nyengine ya uchangiaji mawazo ambapo mada ni tofauti.

Kundi litakapo tambua malengo yake,litakuwa limelijibu swali la kwanza kati ya maswali manne muhimu:
  • Twataka nini?
  • Ni nini tulichonacho?
  • Tutatumiaje tulichonacho kupata tunachotaka?
  • Ni nini kitatendeka, tukifanya hivyo?

Maswali hayo manne, yana umuhimu mkubwa katika usimamizi, kwa hivyo, pia katika uwezeshaji wa jamii (kwa sababu hiyo, yamechaguliwa kama mada katika vikao hivi vya kuchangia mawazo).

Kwenye mfuatano huu, kikao cha kuchangia mawazo kinatumika kama mbinu shirikishi ya kuyajibu maswali hayo manne kama kundi moja,kupunguza uwezekano wa maswali hayo kujibiwa na mtu mmoja au sehemu ndogo ya kundi au jamii. Katika kuyajibu maswali hayo, ndipo kundi litafanya maamuzi kuhusu mwelekeo utakaochukuliwa na jamii, na kupanga mbinu zitakazo tumika katika utekelezaji.

––»«––

Kikao cha kuchangia mawazo:


Kikao cha kukchangia mawazo

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 09.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Changia mawazo