Ukurasa wa nyumbani
 Katika utendaji




Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Ewe
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
नेपाली / Nepālī
Polszczyzna
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
ไทย / Thai
Türkçe
اردو / Urdu
Èdè Yorùbá

                                        

Kurasa zengine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

MAWASILIANO KATI YA VIONGOZI NA UMMA

Kuweka Uwazi

na Phil Bartle, PhD

translated by Lillian Naka


Maelezo ya mafunzo

Mradi unaofanywa katika jamii, haupaswi kuwa wa siri; lazima jamii hiyo ielezwe kinachoendelea

Katika kazi yako ya kuisanya jamii hiyo,unatakiwa kuwa na uwazi,usiwe dikteta na unahimizwa kuihusisha jamii katika mazungumzo na maamuzi, pia unapaswa kuwahimiza viongozi kuwa na uwazi kwa jamii yao.

Njia tatu muhimu, ambazo zikitumiwa vyema, zitaleta mawasiliano mema kati ya jamii na viongozi wao ni: mikutano, ripoti na uchunguzi.

Mikutano ya hadhara ni njia nzuri ya kueneza habari kati ya viongozi na jamii kwa jumla. (sherehe kama zile zitakazotajwa hapo chini, zaweza kujumuishwa katika mikutano).Katika mikutano, ni vyema kuwahimiza na kuwajuza viongozi kuchukua jukumu la "Msahalishi" kama ulivyofanya kama mhudumu wa kijamii.

Wanaitajika kuwa waongezi wazuri katika mhadhara, wajiepushe na kutoa hotuba, kufunza au kutoa injili. Wajifunze kupata majibu kutoka kwa washiriki.Njia hiyo ya mawasiliano kwa pande zote mbili, ("maongezi" ni pande mbili) itasaidia kuongeza uwazi na kuimarisha uongozi kwa kushirikiana.

Ripoti ni muhimu pia. Zinafaa luandikwa vizuri na kwa lugha inayoeleweka na jamii, pia inafaa kutangazwa katika mikutano ya jamii. Majibu kutoka kwa jamii ni ya muhimu.

Uchunguzi, ambapo baadhi ya watu kutoka kwa jamii pamoja na viongozi, watatembelea mahali panapo fanyika mradi huo pamoja, kutachangia kuboresha uwazi na mawasiliano mema.

Ujumbe uliochapiswa na kubandikwa mahala tofauti tofauti, utasaidia kusambaza mawasiliano, lakini haufai kutumika peke yake. Vibandiko hivi haviwezi kutumika badala ya mikutano ya hadhara. vibandiko hivyo vyaweza tu kutumika ili kuhamasisha umma, au kutoa ripoti ya matokeo ya mradi.

Ripoti ya matumizi ya pesa inayoashiria vile pesa zilivyo patikana na vile zilivyo tumika, ikibandikwa katika kliniki au shule ikiwa ingali inajengwa, husaidia kuboresha uwazi.

Jambo muhimu kwako kama mhudumu wa jamii hiyo, ni kuhimiza uongozi mzuri, ushirikiano katika kuudhibiti mradi, na uwazi kupitia mawasiliano mema kati ya viongozi na jamii kwa ujumla.

Vile ulivyo jifunza na kuzielewa njia za usahalishi katika uongozi, kutachangia pakubwa vile utakavyo wafunza na kuwahimiza viongozi kuzitumia njia hizo.

������

Mkusanyiko wa jamii:


Mkusanyiko wa jamii

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
������
Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Katika utendaji