Ukurasa wa nyumbani
 Uhamashishaji




Fasiri:

বাংলা / Baṅla
Català
中文 / Zhōngwén
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Polszczyzna
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
Tiếng Việt
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

MAFUNZO KAMA UHAMASHISHAJI

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Wamalwa Philip


Kijitabu cha Mafunzo

Mbinu za kukuza usimamizi wa jamii hujumulisha mbinu za maendeleo ya jamii na mafunzo ya usimamizi wa jamii

Maana Yetu Maalum ya "Mafunzo:"

Neno "mafunzo" mara nyingi hufukiriwa kuwa ni kutoa ujuzi kwa wanafunzi. Kutia moyo mwanafunzi huonekana kama ni jambo la kando tu. Katika mafunzo ya usimamizi wa jamii, jukumu lake ni zaidi ya ile ya kuondoa umaskini na kujenga uwezo wa jamii. Pia imeundwa kuhamashisha kikundi hicho kuchukua hatua mwafaka na usimamizi kuongeza uwezo na nguvu.

Vipengele muhimu ya neno mafunzo katika maana hii maalum in pamoja na:
  • Kufahamisha;
  • Kutoa habari;
  • Kusambaza Ujuzi;
  • Kusisimua au kutia moyo;
  • kuhamashisha; na
  • Usimamizi.

Ni vipengele viwili vya mwisho ndivyo vinafanya mafunzo haya yawe maalum; mafunzo KAMA uhamashishaji, si tu mafunzo KUHUSU uhamashishaji.

Kufahamisha:

Mafunzo hutumika kama njia ya kuongeza ufahamu wa jamii kuhusu maswala kama ya kijinsia, usafi wa mazingira, mafundisho kwamba umaskini si kusudio la Mungu au Majaliwa mbali ni kitu ambacho kinaweza kubadilishwa na watu ikiwa wako tayari kuchukua hatua zifaazo.

Kuhamashisha katika mafunzo ya usimamizi wa jamii inajumulisha kuvifahamisha vikundi vilivyolengwa kuwa sisi sio msaada wa kutegemewa mbali tunatoa mafunzo ambayo yatawasaidia hao wajisaidie wenyewe.

Kutoa Habari:

Ikiwa kutoa ufahamu utapelekea watu kuelewa vyema shida zinazowakabili (kwa mfano kwamba hakuna usawa wa kijinsia na ambayo inazuia maendeleo), mafunzo huongezea kwa matokeo hayo ya ufahamu kwa kutoa habari kuwa kuna suluhisho kwa shida hizo, ikiwa tu vikundi vya washirika waliofundishwa vitakua tayari kuchukua hatua.

Kusambaza Ujuzi:

Maana ya kawaida ya "mafunzo," kwa mara nyingi huangazia tu kipengele hiki cha kusambaza ujuzi. Hii humaanisha kuwa mwalimu hugawa ujuzi kwa wanafunzi. Maana maalum ya mafunzo haitengi kipengele hiki cha kusambaza ujuzi, mbali inaangazia kwa makini zaidi vipengele vingine vya mafunzo.

Ijapokuwa ujuzi kama wa useremala na uashi au ujenzi ni muhimu, ujuzi huo hauhitajiki kwa dharura katika jamii. Kile ambacho kinahitajika zaidi ni ujuzi wa kuhamashisha, wa kupanga, kutambua rasilimali, kutambua matakwa na vipao mbele vya jamii, kuunda miradi, kuandika mapendekezo na kuripoti (uazi). Kusambaza ujuzi huu wa usimamizi ni moja ya malengo makuu ya mafunzo ya usimamizi wa jamii.

Kusisimua:

Kutia watu moyo ili wajichukulie hatua wenyewe na wala sio tu kutumaini na kugonjea msaada kutoka nje, hufanywa kwa kuvifahamisha vikundi vinavyofundishwa kuwa vina haki (au hata jukumu) na uwezo wa kubadilisha vitu viwe vizuri.

Wanafahamishwa kuwa wana mali yao na vipawa vyao, sio kulaumiwa, na wanapongezwa kwa mafanikio yao. Huku kutia moyo hafanya watu kuwa tayari kuchukua hatua kwa niaba yao wenyewe na hata kwa niaba ya jamii zao.

Ikiwa kikundi au jamii imetiwa moyo zaidi, basi ni imara zaidi. (Tazama Vipengele vya Kukuza Jamii).

Na, hasa:

Uhamashishaji na Usimamizi:

Kipengele muhimu cha kufanya jamii iwe na uwezo zaidi ni kwa jamii hiyo kufanya vitendo. Kuunda tu vikundi (na vyeo vya Mwenyekiti, Makamu, Mweka Hazina na Katibu kwa mfano) si kitendo cha kutosha, hiyo ni njia ya kuandaa jamii kufanya jambo. Kuhamashisha kunamaanisha kufanya jambo litendeke na matokeo kuonekana. Kwa hivo kujiandaa ili kuwezesha jambo fulani kufanyika ni jambo muhimu katika mafunzo ya usimamizi.

Hii ni mbinu ambayo inaleta pamoja mbinu kutoka nyanja mbali mbali, (1) usimamizi wa vyama vya kutetea wafanyikazi na (2) mafunzo ya usimamizi wa maafisa wa ngazi za juu wa makampuni kubwa kubwa. Yote mawili hayalengi tu kusambaza ujuzi kwa mtu binafsi mbali katika kuunda vikundi vyenye uwezo na mafanikio makubwa. (Ili kujua tofauti kati ya kujiandaa kwa ajili ya kutoa maamuzi na kujiandaa kwa ajili ya kufanya kitendo, tizama sehemu ya mafunzo ya Usimamizi).

Washiriki wa mafunzo haya sio tu wanafunzi ambao wanapata ujuzi na habari. Ni washiriki ambao tayari ni sehemu ya shirika, au wanatarajiwa kuwa sehemu ya shirika kwa sababu ya mafunzo haya. Mafunzo hutumia mitindo kama ya "kuchangia mawazo"

(Tazama: Njia za Kuchangia Mawazo) ili kupata kutoka kwa washiriki hao nia na malengo ya kikundi, na njia bora zaidi ya kukiendesha kikundi kwa (1)kufanya maamuzi, na (2) vitendo. Matokeo ya mafunzo hayo sio tu kuwa wanafunzi wanajua zaidi na wenye ujuzi lakini kutayarisha washiriki ambao wameandaliwa na kuhamashishwa kufanya vitendo.

Mafunzo ya jamii ya usimamizi imetumia hayo kwa kukuza na kuwezesha jamii.Tazama Mafunzo ya Usimamizi Kwa ufafanuzi zaidi juu ya vipengele mafunzo vya uhamashishaji na usimamizi

––»«––

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011

 Nyumbani

 Uhamashishaji