Tweet Tafsiri:
'العربية / Al-ʿarabīyah |
UTARATIBU WA MBINU ZA JINSIAMwandishi Phil Bartle, PhDMtafsiri Caroline NdururiVidokezo vya MhamasishiUtaratibu wa mhamasishi wa kuinua ufahamu na usitawishaji wa usawa wa kijinsiaMuhtasari: Huu ni utangulizi wa baadhi ya masuala kuu ya kijinsia, na baadhi ya mbinu zinazoweza kutumiwa na mhamasishi wa jamii. Utangulizi: Maandiko haya, kama yanayopatikana kwenye tovuti hii, yameelekezwa kwa mhamasishi wa jamii, na siyo maandishi ama makala ya taaluma. Lengo lake ni kujulisha mhamasishi kuhusu masuala yanayohusiana na jinsia, na kumsaidia kukuza maarifa ili kuleta ufahamu kuhusu masuala ya kijinsia na kuelimisha jamii na mashirika yao kuhusu uongezeko wa usawa wa kijinsia na haki. Mheshimiwa, Mary Nagu, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Maswala ya Wanawake na Watoto,Tanzania,alisema, ''Hatuwezi kupata maendeleo ya jamii iliyo halisi bila usawa wa kijinsia, ushiriki wa jamii ndio elementi ya muhimu kabisa kwa kutekeleza usawa wa jinsia.'' (Personal Communication, Istanbul, 1996) Kwa kweli, kazi ya jamii ni chombo muhimu cha kuleta uinuo wa ufahamu kuhusu maswala ya kijinsia, na cha kusawazisha baadhi ya tafauti. Jinsia Dhidi ya Aina: Baadhi ya wasimamizi sugu wa kuhimili dhuluma dhidi ya wanawake wanasema neno ''jinsia'' si neno halali,iliundwa tu kutaabisha vikao vya kiasili. Bali na haya, ni muhimu kwa mhamasishi kujielimisha kuhusu neno ''jinsia'', kwa sababu gani inatumiwa, na umuhimu wake kwa ujenzi wa uwezo,uzalishaji wa mapato na kuwawezesha jamii wenye mapato ya chini. Kwanza kabisa ni kutofautisha kati ya maneno ''aina'' na ''jinsia.'' Kwa ufupi, ''aina'' ni kiubiologia na ''jinsia'' ni kiushirika. Sifa za kiubiolojia zinaenezwa na kudumishwa katika vizazi kupitia majeni (na uzazi wa kingono) ilhali sifa za kiushirika zinafunzwa, kuenezwa na kudumishwa (na viashirio wala sio majeni) kupitia mawasiliano na utaalamu (uzazi wa kiushirika). Tafauti kubwa katika aina ni kati ya ''mwanamume'' na ''mwanamke'' ilhali kwenye jinsia ni kati ya ''ume'' na ''uke''. (Utafiti wa kiubiolojia unadhihirisha ya kwamba tunaweza kumiliki zaidi ya aina mbili, pengine kadiri ya miungano tano tofauti za kromosomu X na Y na jeni zao. ''Ume'' au ''uke'' unatafauti sana, na hutofautiana kutoka utamaduni kwa utamaduni, na enzi kwa enzi katika historia. Sentensi hii inadokeza ya kuwa sifa za ushirika (ume au uke) ambazo wanadamu hutumia kwa watu tofauti, kama kiitikio kwa sifa zao za kiubiolojia, ni holela kiutamaduni, na zinaweza kubadilishwa katika mfumo wa maendeleo ama mageuzo mengine ya ushirika. (Sifa zetu za kiubiolojia zinatambulishwa kwa wingi na urithi wetu wa ujeni, na zinaweza kubadilishwa, kwa ugumu, kupitia upasuaji, madawa, ama kupitia njia zingine za kibinadamu). Masuala ya Haki za Binadamu: Ijapokuwa maadili yanatofautiana kutoka jamii kwa jamii, nchi kwa nchi na mara kwa mara, tunaweza kukiri ya kuwa kuna maafikiano, kwa jumla, kuhusu wema na uovu. Ubaguzi wa rangi ni dhana yenye upana na kwa jumla inachukuliwa kuwa ovu, ijakapokuwa kuna uwezo wa kutambua watu wenye maadili ya ubaguzi.Itikadi yenye maana kwenye ubaguzi wa rangi ni kwamba kuna watu wanaotambuliwa na baadhi ya sifa za kimwili (rangi ya ngozi, nywele muundo wa mfupa) na mbaguzi anaamini ya kwamba hizo sifa za kimwili hufunga watu kwa tabaka, na kwamba baadhi ya sifa zisizo za kimwili zitatumika wazi kwa wote walio katika tabaka hiyo. Baadhi ya itikadi za ubaguzi za wazi ni (1) ''Wanegro wote ni wenye asili ya kimuziki'', (2) ''Wazungu wote ni wabaguzi wa rangi'', (3) ''Wayahudi wote ni wajanja na pesa'', ama (4) ''Watu fulani ni makauleni, malaya, mabahili, ama wenye njaa ya mamlaka,'' - na kadha wa kadha. Itikadi hizi za ubaguzi hutajwa mara nyingi kuhalisisha dhuluma kwa baadhi ya watu kwa njia ya ubaguzi, ama kuhalisisha sheria zinazotungwa kuzuia ushiriki wao kamili katika maisha ya kiraia. Inapochunguzwa, inakua wazi kuwa ubaguzi wa kijinsia ni sawa kama ubaguzi wa rangi. Ni ubaguzi wa sifa zisizo za nje za ushiriki, na mienendo kwenye, vitengo vya watu wenye baadhi ya sifa za kiubiolojia. Tukiangalia kwenye maafikiano kati ya mataifa kama vile Ilani ya Haki za Binadamu, tunaweza kupata maadili ya manufaa kwetu. Baadhi yao ni wazo kwamba kila mtu ana haki ya huduma, uweza, huduma za kisheria, ama ushiriki wa kiraia, bila ubaguzi wa rangi, itikadi za kidini, ama babu nyingine zinazogawanya ubinadamu. Mashinani, kwenye watu walio na mapato ya chini na elimu hafifu, jamii ambazo tunazoawazwa, maadili haya ni geni, na hata mara nyingi hayajulikani. Hii huweka mzigo wa jukumu kwa mhamasishi; kufunza maadili haya, na kufanya kazi, kama makaimu wa mageuzi, kwa kutekeleza maadili haya ya kiulimwengu, kama baadhi ya utaratibu wa uhamasishi. Masuala ya Kiuchumi na Kisiasa: Binadamu wote wanaweza kuchangia katika jamii zao kwa njia na viwango tofauti. Jamii huimarishwa na hizo michango, kwa sababu, na si juu ya, hizo tafauti. Kama ni mazoea ya kikundi cha watu kutoshirikisha kama asilimia hamsini ya umma kwa shughuli za mazao; basi uchimbaji wao wa shughuli za kiuchumi huzorota kwa kupoteza asilimia hamsini ya mazao inayotarajiwa. Kwa sababu ya athari ya kichanganyiko,asilimia hamsini ya mazao hayo yakiunganishwa, uchimbaji utazidi asilimia hamsini iliyoongezwa, labda itaongezeka kwa mara tano zaidi. Kutoshirikisha nusu ya umma kwa sababu ya jinsia inaathiri uchumi kwa asilimia hamsini zaidi. Kiuchumi, ni hekima kushirikisha wanawake na wanaume kwa usawa katika uchumi wa jamii yoyote. Alhasil, kama ni mazoea ya kikundi cha watu kutoshirikisha asilimia hamsini ya umma kwenye uamuzi ya kisiasa yanayoathiri jamii yote, basi uwezekano wa uamuzi hupungua. Dhana inayoshikiliwa na jamii kuhusu hali ya baadaye na uwezo wake hukadirika. Thamani hupotea. Ni hekima kushirikisha wanawake kwa usawa kwenye utaratibu wa uamuzi wa kisiasa wa jamii yoyote. Njia ingine ya kuona na kuelewa hasara hiyo ni kutoshirikisha wanaume kwenye shughuli za kiuchumi ama utaratibu wa uamuzi wa kisiasa. Kisayansi, hakuna sababu yoyote kudhania ya kwamba chango la wanaume ni bora ama zaidi kwa njia yoyote kuliko chango la wanawake. Watu wasioshirikishwa barabara (kwa mfano wanawake) kwenye mfumo wa kisiasa na uchumi hubuni rasilimali ya thamani isiyofaa kudharauliwa katika maendeleo ya jamii. Umaskini utazidi bila hao. Kisiasa na kiuchumi, jamii itakua imara zaidi, ya anuai zaidi, ya bunifu zaidi, ya mazao zaidi, ya usawa zaidi, wanaume na wanawake wakipewa nafasi sawa kushiriki katika maisha yake ya kiuchumi na kisiasa. Masuala ya Kiutamaduni: Kwenye warsha ya kijamii iliyosahalishwa na wanawake wawili wachanga kutoka Wizara ya Jinsia ya Uganda (kwa niaba ya mradi wetu wa kuwezesha jamii), Nilimskia mzee mmoja akilalama, ''Mnajaribu kuua utamaduni wetu?'' Alikua na uhakika ya kwamba ni kimila na kiutamaduni wanawake kuchukulia wanaume wote kuwa wakuu kwao, kwamba wanawake hawafai kushiriki kwenye utaratibu wa uamuzi wa kijamii, na kwamba jukumu la wanawake ni kuhudumia wanaume. ''Hapana,'' mwanamke mchanga alijibu mbele ya mkutano, "Hatuathiri utamaduni wetu" Tunataka kuimarisha sehemu zake bora na kutupilia mbali sehemu zisizo na manufaa.'' Wewe, kama mhamasishi unahitaji jibu kwa wale wanabishania kuhifadhiwa kwa utamaduni wao, wale wanahofu ya kuwa ukigeuza desturi na vikao chache basi utaangamiza utamaduni huo. Anza na ufahamu wa maana ya utamaduni. (Rejea asili ya utamaduni katika makala, Utamaduni). Utamaduni una uhai (kidubini), ushirika kuliko kiubiolojia. Una mambo yote (vikao, miendo, itikadi) yanayofunzwa kuliko kurithiwa kiujeni. Lazima ikue na ibadili ili ibaki hai. Kukua na kubadili inamaanisha mageuzi. Chochote ambacho kimehifadhiwa hakina uhai. Dagaa lazima wafe ili wahifadhiwe kwa kebe... Achali ndani ya chupa ya kuhifadhi hayana uhai. Vifaa ndani ya jumba la makumbusho havina uhai. Hivi vitu vyote havina mageuzi, ndio kwa maana vinahifadhiwa. Sisi kama wahamasishi tunaheshimu na kuadhimisha mila na utamaduni wenyu/wetu. Tunauona utamaduni wetu ukiwa na uhai, lakini, si ule hauna uhai (hauna mageuzi) kama lugha ya Kirumi. Lakini, kwa utamaduni wetu wa heshima uhifadhiwe, lazima ukue na ubadili; Kwa hivyo, lazima ugeuke ili ufikiane na mazingira ya kisasa ya dunia. Mageuzi hayawezi kuepukika. Ijapo lazima kuwe na mageuzi, basi ni vizuri kuwe na athari kuhusu mwelekeo wa mageuzi hayo badala ya kuyatambulisha kiutamaduni bila ya ushiriki wetu. Ijapo lazima sheria zetu zibadili, basi ni vizuri zibadili kuelekea kwenye ilani ya ulimwengu kuhusu haki za binadamu badala ya sheria ya kimwitu. Kwa muda mfupi, kusawazisha ushiriki wa kijinsia unaweza kuonekana kuwa kinyume na utamaduni, sanasana ambako wanawake walikuwa wamedhulumiwa. Kwa muda mrefu, kwa kinyume, ushiriki wa sawa wa wanaume na wanawake utachangia katika jamii imara, na kwa hivyo katika uthabiti,maendeleo, na uhifadhi wa utamaduni wetu. Ilhali sehemu nne zilizotangulia zilifafanua asili ya jinsia kwa ushirika na kiutamaduni na hoja ya kuboresha usawa wa kijinsia ili kuimarisha jamii, sehemu zifwatazo zinakuagiza jinsi ya kuunda mikakati zako mwenyewe, kama mhamasishi, kwa kuzisaidia na kuongoza jamii katika kutimiza usawa wa kijinsia zaidi na ustahiki. Mwinuko wa Ufahamu: Kusuluhisha tatizo, lazima tufahamu kama lipo. Kumbuka ya kwamba washiriki wa jamii lazima wasuluhishe matatizo yao ya kiushirika na kiujamii. Kama katika maendeleo ya jamii yote, hauendelezi jamii, jamii inajiendeleza. Maingilio yako, pamoja na mwongozo, usisimuo, elimu na usukumizi, unaweza kuleta mwelekeo, lakini mabadiliko yanafaa kutekelezwa na washiriki. Washiriki wengi hawawezi kuona kuna tatizo la kusuluhishwa, ama hawataki kuliona. Washiriki wengi hufaidika katika mamlaka hasiyo na usawa na wanaogopa mabadiliko yoyote yanayoweza kupunguza mamlaka yao, ufahari, makadara ama mafao yao ya kiuchumi. Wale, walio na masilahi ya kiubinafsi kama hayo, watanena ya kwamba hakuna tatizo lolote, ama wagombane kuwa kubadilisha mila na itikadi za kiasili utaathiri utamaduni. Jawabu lako kwa tatizo la kwanza ni utetezi, mwinuko wa ufahamu na kuelimisha washiriki wote wa jamii. Kwa la pili, kukabiliana na masilahi ya kiubinafsi itazingatiwa kwenye sehemu ifwatayo. Utaratibu wa mwinuko wa ufahamu miongoni mwa kikundi kilicholengwa unatatuliwa kwa ubora na mbinu za shirikishi. Kumbuka ya kwamba tunaelimika kwa uchache kwa kusikiza, kwa kiasi kwa kutazama utendaji, na zaidi kwa kuhusika - kwa kutenda. Kumbuka washiriki wa jamii watachukua jukumu zaidi kwa mradi wakikata hukumu la kuitekeleza, na wasipochukulia imetozwa kwao kutoka nje. Lazima ''wamiliki'' mradi huo. Hizi ni kanuni za msingi za maendelezo ya jamii kama zilivyofafanuliwa kwenye Mwongozo wa Wahamasishi. Mbinu yako kuu, basi, ni kwenye vikao vya vikundi, kuuliza maswali, kama Socrates. Usihubiri, ubishane, ama kuhutubia washiriki. Waulize maswali yatakaowaongoza kuangalia uhali, jamii yao, kwa mipaka ya usawa wa kijinsia. Lakini, haitaumiza kujumuika kibinafsi na watu wenye nabihi, rehema na wakidini na viongozi wengine wa maono na jamii, na kuwahimiza kuhubiri, kuhutubia ama kubishana kuhusu mada hiyo. Maswali kuhusu usawa wa kijinsia hayafai kuachiwa warsha maalum zinazohusika na jinsia pekee (zinazokinga suala hilo, na mara nyingi huwa kama kuhutubia waongofu), bali yanafaa kuhusishwa barabara katika elimu ya uongozi na uhamasishi wa jamii kutekeleza miradi yao wenyewe. Usitawishaji wa Usawa wa Jinsia: Kuna tafauti za usawa kuu zenye haziwezi dhibitiwa kwa dunia halisi, ambamo wanaume wanapatikana kwa wingi katika hali fulani na wanawake kwa hali nyingine, kwa ujumla zinazowadhulumu wanawake kinyume na wanaume. Lengo la usawa wa jinsia litakua lenye kurekebisha tafauti hizo kuu. Kiwango madhubuti cha asilimia hamsini kamili cha kila hali kitakua yabisi, na kigumu kufanya kazi nacho. Baada ya kuona ya kwamba tokeo la usawa wa kijinsia linaambatana na thamini zetu za haki za binadamu, na linafaidi utamaduni wetu, kisiasa na kiuchumi, basi lazima tuulizie mbinu tunazoweza kumiliki kulitekeleza. Huu si wakati wa kumiliki mbinu ya, kujaribu kutumia, kwote, njia wastani ya sahihisho. Kuna umuhimu wa kuchanganua kila tatizo na kutafuta utambuzi wa kienjeji ufaalo kila tatizo. Catalina Trujillo, mradi wa UNCHS wa Wanawake kwenye Makazi, alitumia mandhari inayojulikana sana katika muktadha wa lengo hili: ''Tafakari kiulimwengu - Tenda kienyeji'' Tazama UNCHS Mageuzi ya ushirika ikidhamiriwa, unaweza kupata watu wanaounga mkono mageuzi hayo na wanaoyapinga. Tatizo hili kuhusu uongezeko wa ushiriki wa jamii, kwa mfano, linapatikana kwenye mwongozo wa wahamasishi. Watu wanaopinga mageuzi huwa ni wale walio na masilahi ya kiubinafsi. La ajabu ni kuwa wale walio na uzuizi watayapinga mageuzi hayo, na ni kwa sababu wanaamini watapata hasara, hata kama hautafahamu thamani ya hasara hiyo. Watu waliodhulumiwa mara kwa mara hukatalia kwenye minyororo hiyo kwa sababu wanadhani watapoteza ulinzi na fursa ya kuchukua jukumu na kufanya maamuzi. Watu wanaoona ya kwamba watafaidika kutokana na mageuzi hayo ni wandani, ama wanaweza kuwa wandani wako na wa watu wengine wanaotaka kutekeleza mageuzi hayo. Mbinu zako, kwa hivyo, nizakudhihirisha ya kwamba mageuzi yaliyopendekezwa niyakunufaisha watu wote, mpaka wale wanaodhani watapata hasara. Mageuzi yanafaa kuonekana yenye manufaa kwa wale wanaoweza kuyapinga ili waweze kuondoa upinzani wao, na hata waunge mkono mageuzi hayo kwa uhodari. Kwa dhana ni rahisi, lakini ina ugumu wake. Kifano kingine ni kwenye kuratibu shirikisho la wafanya biashara. Kwa kuratibu shirikisho, wanachama wote watafaidika kwa kupata ujira na kanuni za kikazi bora, wakijiunga na shirikisho hilo. Jambo moja unalojua, amabalo lilifafanuliwa hapo awali, ni kwamba jamii itafaidika kwa ushiriki wa wanaume na wanawake. Kuondoa vizuizi kwa ushiriki wa aina yoyote ya watu itamaanisha kuwa mazao (kisiasa, kiutamaduni,kiuistlahi, kiuchumi) yatakua na tafauti zaidi, msingi zaidi, na ubuni zaidi. Kwa jumla kutakua na uhamasishi (uwezo utaongezeka), na washiriki wote watafaidika. Hakutakua na matatizo yoyote kuwasiliana na watu walio na ufahamu zaidi wa ushirika na siasa. Kwa hivyo uhamasishi wako, ilivyotajwa hapo mbeleni, haupaswi kuhusika na tafauti pekee, bali hata ufafanue faida za uongezeko wa usawa wa kijinsia kwa ujumla na kwa kila mshiriki. Kanuni ya msingi ni kwamba sera inayozingatia wote itakua na manufaa kwa jamii na washiriki wake. Ufululizo wa Jinsia: Mbinu inayotumiwa mara kwa mara katika mageuzi ya ushirika ama kwenye miradi ya maendeleo, ni kuanzisha mageuzi hayo katika sehemu ama sekta moja, kisha, juu ya ufanifu na mafunzo inayopatikana, kuyafululiza katika jamii yote. Kwa kazi yako,uhamasishi wa jamii, upungufu wa umaskini, usahalishaji wa maendeleo ya uwezo ya mashirika, mafunzo ya wasimamizi, usitawishaji wa kujitegemea, mbinu hiyo ya ufululizo haifai. Mfululizo wa ufahamu wa kijinsia na usitawishaji wa usawa wa jinsia zinafaa kuhusishwa mwanzoni mwa kazi yako na kutekelezwa mpaka mwisho. Tatizo la kushugulikia jinsia mwanzoni katika sehemu kadhaa,ilivyofafanuliwa, husababisha ukingaji wa masuala. Ukiandaa warsha ya kijinsia, utawavutia zaidi washiriki wanaofahamu tatizo hilo na wanaounga utatuzi. Ukishirikisha ufahamu wa jinsia na kutunga mbinu za usawa wa kijinsia kama mada mahsusi kwenye vikao vyako vyote vya mazoezi, utafaulu kuwashirikisha watu wanaofaa na ujumbe huo. Warsha inayozingatia jinsia pekee itakua na umuhimu unaporatibu Mafunzo ya Wafundishaji ama unapokua na mkutano na wafanyikazi wako ama watu wakujitolea; basi unafaa kujihusisha na ustawishaji wa mbinu badala ya mwinuko wa ufahamu. Hautakua ukitekeleza mbinu ya kijinsia, bali utakua ukitayarisha wafanyakazi wako na wanaokuunga katika kupanga mbinu ya kijinsia. Kwa harakati zako zote,uhamasishi wa jamii, utungaji wa vikundi, mafunzo ya wasimamizi, maendeleo ya uwezo, upunguo wa umaskini, unahitaji kuhusisha mwinuko na usawa wa kijinsia. Ufululizo unafaa kushirikishwa mwanzoni. Kimalizio: Mwinuko wa ufahamu wa kijinsia na usitawishaji wa usawa wa kijinsia ni sehemu muhimu wa uhamasishi, mafunzo ya wasimamizi, maendeleo ya uwezo na upunguo wa umaskini. Unahitaji kuunda mbinu mahsusi,tambua wale wanaoweza kupinga mageuzi hayo, wafafanulie manufaa kwao, na uhusishe haya yote mwanzoni mwa kazi yako. Hakuna utaratibu mahsusi ama seti ya harakati za kufuata. Unahitaji kuchunguza tatizo, utumie kanuni zinazopatikana katika makala haya, na utengeneze mbinu ya kienyeji itakayokua na fanaka. ––»«––Warsha © Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Sahifa Kuu |
Jinsia |