Ukurasa wa nyumbani
 Uhamashishaji




Fasiri:

Bahasa Indonesia
বাংলা / Baṅla
Català
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Polszczyzna
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
Tiếng Việt

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana


Yaliyomo:

  1. Mwanzo
  2. Utangulizi
  3. Kufanya kazi na jamii
  4. Uliza maswali
  5. Husika
  6. Inua hadhi
  7. Unga mkono wanachama wa jamii
  8. Uchunguzi
  9. Vikundi vya kulengwa
  10. Uajibikaji
  11. Shukrani
  12. Mwisho

Yaliyomo:

  1. Mwanzo
  2. Utangulizi
  3. Kufanya kazi na jamii
  4. Uliza maswali
  5. Husika
  6. Inua hadhi
  7. Unga mkono wanachama wa jamii
  8. Uchunguzi
  9. Vikundi vya kulengwa
  10. Uajibikaji
  11. Shukrani
  12. Mwisho

Yaliyomo:

  1. Mwanzo
  2. Utangulizi
  3. Kufanya kazi na jamii
  4. Uliza maswali
  5. Husika
  6. Inua hadhi
  7. Unga mkono wanachama wa jamii
  8. Uchunguzi
  9. Vikundi vya kulengwa
  10. Uajibikaji
  11. Shukrani
  12. Mwisho

MPANGILIO KATIKA MAENDELEO YA JAMII

na Njia ya Kuhakikisha Usalama wa Chakula

na David Stott

imehaririwa na Jac Slik

imetafsiriwa na Wamalwa Philip


Kijitabu cha Marejeleo

Kuanzisha mifumo mipya ya jamii na uchumi

A. Utangulizi:

Yafuatayo ni maoni juu ya kuanzisha uvumbuzi na mifimo mipya ya kijamii na uchumi katika jamii. Yametokana na uzoefu wangu wa miaka 30 nikifanya kazi kama mkuzaji au mstawishaji wa jamii lakini haswa maoni haya yamemulika uzoefu wangu wa miaka 2-3 iliyopita. Makala haya hayajaandikwa ili yawe kama kitabu cha mwongozo cha "jinsi ya" kufanya mambo yote, lakini yameandaliwa kama mchango wangu kuhusu ustawi wa jamii ambao unaweza kufanikiwa katika eneo moja na kushidwa katika eneo lingine.

B. Kufanya kazi na jamii:

Uamuzi wa ni lini kuanzisha mambo na mipango mipya katika jamii ni jambo ambalo labda lahitaji usanii kuliko ujuzi wa kisayanzi. Nimejionea katika uzoevu wangu wa miaka mingi kuwa kuna nyakati nyingi ambapo sikuweza kufanya maamuzi bora ya wakati wa kuanzisha miradi mipya.

Mstawishaji wa jamii (na mfadhili) wanaweza kugundua jambo la muhimu au linalokera jamii na wakaamua kuleta mabadiliko katika jamii hiyo. Lakini ikiwa jamii ambayo unanuia kuleta mabadiliko haitaki kushiriki katika mabadiliko yanayokusudiwa, basi mradi huo heunda usifanikiwe au kwa bahati, ufanikiwe kidogo tu.

Makosa ambayo nimeona mashirika au watu binafsi wakifanya ni kuamua wao wenyewe kwamba jambo fulani lazima lifanywe, na kwasababu wanafikiri kuwa hawo ndio "wanajua sana" chakufanya (si wanalipwa kufanya hivyo, au sio?), wanaendelea mbele na kujaribu kufanya walilofikiria. Haya huweza kueleweka ikiwa wanataka kuonyesha uajibikaji kwa sababu wasipofanya hivyo huenda wakapoteza ufadhili wao. Lakini fikra hii hutupilia mbali kuhusika kwa jamii na hivyo hupelekea mradi wa mstawishaji wa jamii kushidwa.

C. Uliza maswali ili upate kufahamu jamii:

Mstawishaji anawezaje kuafikia matakwa na shida za jamii? Mstawishaji wa jamii mwerevu ataanza kwanza kwa kujiuliza maswali kama haya:

  1. Je, hili ni "wazo ambalo wakati wake wakutekelezwa umefika" au ni wazo ambalo mstawishaji wa jamii anafikiri lazima tu litakubaliwa na kupokelewa vizuri?
  2. Je kuna malalamiko ya watu katika vyombo vya habari na katika mazungumzo ya watu wa kawaida kuhusu ya swala hilo?
  3. Je, hii ni moja tu kati ya maswala na shida nyingi zinazokera jamii hiyo? Ikiwa ni hivyo, tutawezaji kuiwasilisha vyema zaidi?
  4. Je, watu wanajihisi kuwa wanyonge sana kiasi cha kutoweza kufanya kitu kuhusu swala hilo au wako tayari kufanya jambo fulani aidha kibinafsi au kwa ushirikiano na wengine?
  5. Je ni watu gani wanaonyesha nia ya kufanya jambo fulani na ni watu gani aidha wanakataa, hawajali au wanalalamika tu lakini hawako tayari kufanya kitu kuhusu jambo hilo?
  6. Ni nani katika jamii ile ambao wameheshimika kama watu wenye ushawishi mkubwa wa maoni ya jamii? Wanawezaje kuhusishwa kwenye mradi huo?
  7. Je kuna haja ya kuhamashisha watu kwanza ili kuwatayarisha kuchukua hatua?

D. Husika katika jamii:

Narudia nikisisitiza kuwa ni muhimu sana kwa mstawishaji wa jamii awe na ufahamu mzuri, kuidhamini na kuiheshimu jamii ambayo anaitumikia.

Ikiwa hauijui jamii ambayo utafanya kazi nayo basi fanya hima uwajue watu na kuunda uhusiano nao. Jiunge na vikundi vya eneo hilo, hudhuria mikutano na mikusanyiko ya watu ambao utafanya kazi nao au wale ambao maoni yao ni muhimu kwa ufanisi wa mradi huo.

Ikiwa unatoka katika jamii hiyo lakini unafahamu sehemu au eneo fulani tu, jaribu sana kujihusisha na sehemu ambazo huzifahamu au fanya kazi na watu kutoka maeneo hayo.

Ikiwa hujui lugha ya jamii hiyo, lugha yoyote ile inayozungumzwa hapo, (na kuna lugha nyingi kadiri ya idadi ya jamii zenyewe), jifundishe na uitumie katika kwa kuzungumza na kuandika.

Ndio, inahitaji muda na bidii; lakini usispoijua lugha yao, huwezi kupata heshima na ushirikiano wa watu hao.

E. Inua hadhi ya swala linalokera jamii hiyo:

Kazi yako ni kuanzisha au kuunga mkono swala hilo kwa njia ambayo watu wanaweza kuielewa vizuri na kuhisi kama inawahusu wao.

Kwa mfano, katika miradi ambayo nilihusika nayo, niligundua kuwa kamati tekelezi iliweza kuinua hadhi, hamu na imani katika maswala mawili tofauti: makazi au nyumba na chakula. Hii iliwezekana kwa kuandaa maonyesho ya Makazi/Nyumba ya Bei Nafuu katika soko moja mwaka wa 1997 na sherehe ya Chakula Kilichozalishwa Nchini ambapo palikuwa na maonyesho, maelezo na habari na jaribio la soko la mkulima ilioandaliwa mwaka wa 2006.

F. Wasaidie watu wa jamii wakati wameanza kulitatua tatizo hilo:

Lazima uwe tayari kuunga mkono jamii kuhusu swala fulani kwa kila njia ambayo wako tayari kuitatua, bora tu njia hizo ni halali kisheria na zina uwezo wa kuleta mafanikio.

Kazi yako si kuwa mtaalamu au kiongozi, mbali kupeana maoni, mawazo na usaidizi mahali ambapo inahitajika na kwa njia ambayo watu wanaweza kuikubali au kuikataa kwa urahisi.

Chunga usifungwe macho na matarajio na malengo yako mwenyewe.

G. Tumia uchunguzi na vikundi maalum vinavyolengwa ili kutambua shida
na uwawezeshe watu wa jamii hiyo:

Njia moja ambayo hutumika sana kukusanya habari ni kwa kufanya uchunguzi au utafiti ili kujua maoni ya watu kuhusu swala fulani. Njia nyingine ya kujua maoni ya watu ni kupitia kuunda na kulenga vikundi vidogo vidogo.

Hata hivyo, njia zote hizo ni muhimu. Mbinu hizi zitakuwa za mafanikio zaidi ikiwa zitafanywa kwa namna ambayo itawaimarisha na kuwezesha watu badala ya kuwatumia tu kama njia ya kupata habari.

Kwa hivyo usiwaalike watu waje tu kutoa maoni yao mbali pia waulize ikiwa wangependa kushiriki katika utekelezaji wa mapendekezo waliotoa na halafu pia uwaulize wafanya hivyo kama wafadhili na wenye kufaidika.

1. Uchunguzi:

Kwa mfano, katika utafiti ambao tulifanya na watu katika mradi wetu wa Benki ya Chakula wa 2006, hatukuwauliza tu maoni yao kuhusu mambo ya chakula, matarajio na shida zao, la. Tuliwauliza pia wachangie maoni yao juu ya njia bora zaidi za kukuza chakula na vile vile mitindo ya upishi. Hakikisha kuwa uchunguzi unapofanywa, ni maswali muhimu tu ambayo yanaulizwa kwa kutumia lugha safi ukizingatia jamii iliyolengwa.

Mwisho, maoni ya watu unayopata kutoka kwenye utafiti utakuwezesha kujua ni nani watakuwa tayari kushiriki katika mradi na "wakati mzuri" wa mradi huo kuanza.

Hata hivyo, ni vigumu sana kujua ikiwa watu wako tayari kushiriki katika mradi kwa kutumia tu matokeo ya uchunguzi. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuwafanya watu kusema wanaunga mkono jambo fulani lakini wasite kuchukua hatua (kwa mfano kwa kutaka tu kusema "jambo nzuri", kukosa wakati au hamu ya kushiriki kikamilifu au kujisikia hawana uwezo wa kufanya kitu kuhusu jambo hilo).

2. Vikundi vya kulengwa:

Ni rahisi zaidi kujua na kutatua shida zilizotajwa hapo juu kwa kulenga vikundi vidogo vidogo.

Lakini kuna hatari, nayo ni kwamba wakati mwengine vikundi vya kulengwa huweza kutumiwa kimakosa kama chanzo cha habari bila kuwaalika watu hao kushiriki baadaye katika mradi wenyewe. Naamini kuwa hii ni kuharibu rasilimali na uwezo wa jamii. Hawa watu ni vyema zaidi waalikwe kushiriki katika mradi mzima, ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi.

Kwa mfano, katika mpango wetu wa sasa wa Jamii za Magharibi (ya Canada) za kujitosheleza kwa chakula, tutakuwa tukiwaalika wahusika mbali mbali (kama vile wakulima, wauzaji,wanunuzi, na maafisa wa miji ) kukutana na kujadili kile ambacho kila mmoja anaweza kufanya ili kuongeza uzalishaji wa chakula, mauzo na utumiaji katika eneo hilo. Kila idara itaulizwa kujadili ni nini inaweza kufanya ili kutimiza haya na msaada ambao itahitaji kutoka kwa idara zingine ili kufanikiwa. Hatimaye, vikundi hivi: vitakutana, viunde mpango wa pamoja, vijiwekee malengo ambayo yanawezwa kutimizwa na kuanza kufanya kazi ili kutimiza malengo hayo.

Ikiwa utapa kwamba watu wengi wamejitokeza kukutana na kujadili swala fulani, basi jua kuwa umetambua shida halisi.

Mstawishaji wa jamii mwenye busara atajiuliza, je hawa watu waliojitokeza ni nani, wanatoka katika sehemu gani ya jamii na ni jinsi gani ambayo bora zaidi kuwashirikisha. Ikiwa mradi huo ni wajamii nzima, mstawishaji atakuwa na jukumu la kuviunganisha vikundi tofauti katika jamii hiyo pamoja. Iwapo vikundi au watu hao hawafai au hawataki kufanya kazi pamoja, basi mstawishaji atakua kama kiunganishi kati yao.

Lakini katika mradi unaolenga jamii nzima, ni vyema sana kuhusishwa sehemu au vikundi mbali mbali katika mradi huo kadiri ya uwezo. Katika uzoefu wangu nimeona kuwa kuna watu aina kadhaa, wa kuongea tu na wenye vitendo, na wale wenye maoni na vitendo. Wahusishe wote hao katika njia ambayo kila mtu atachangia mradi.

Onyo: Usijaribu "kuleta jamii yote pamoja" kuhusu swala fulani mwanzoni wa mradi. Ikiwa unashughulika na swala nyeti au maswala mengi kwa pamoja, lazima kutakuwa na maoni mengi katika jamii na huenda usifanikiwe kuleta maelewano na kupata suluhisho. Kwa hivyo, mikutano itakayofuata huenda ikavutia washiriki wachache na idadi hiyo ikaenda ikipungua. Basi ni vizuri kuanza kwanza na kikundi kidogo halafu uende ukiongeza watu na viundi vingine jinsi maswala tofauti yanavyotambuliwa na mipango ya kuyatatua kuundwa.

H. Uajibikaji kwa mashirika fadhili:

Je kama mstawishaji wa jamii, unawezaje kupatanisha nia ya kutaka "kuafikia malengo ya jamii" na jukumu la "uajibikaji" au kutimiza malengo (au hata masharti) ya wafadhili?

Nimegundua kuwa ni lazima tujiwekee malengo (kwa mfano, lengo la 1 -idadi fulani ya watu (ikiwakilishwa na herufi X) ikishiriki katika mradi huu, lengo la 2 - basi mradi fulani Y utaweza kufikia malengo fulani Z kufikia tarehe fulani). Lakini haya lazima yafanywe kwa sharti kuwa jamii itashirikishwa katika kuweka malengo hayo kwa kuwa ikiwa jamii haitataka kufanya hivyo, mradi huo huenda usifanikiwe.

Kwa mfano, katika pendekezo moja la hivi majuzi, niliweza kupata ufadhili wa miradi sita ambayo uchunguzi wetu uliokuwa umeonyesha kuwa watu walihitaji. Mwishowe, tuliweza kukamilisha vizuri tatu kati ya mradi hiyo sita. Shirika lililo tufadhili lilifurahia sana matokeo haya na likaamua kufadhili mradi wetu mwingine katika eneo hilo.

I. Shukrani:

Basi hivyo ndivyo yalivyo kwa ufupi. Nataraji kuwa maandishi haya yalikua yenye manufaa na nakaribisha maoni na mapendekezo ya mtu yeyote. Ningependa kuwashukuru wale wote ambao wamenisaidia aidha kuunda au kutekeleza yale ambayo yamejadiliwa hapa. Hasa, ningependa kuwashukuru Dr. Phil Bartle, John Mitchell na Bernice Levitz Packford; lakini zaidi, shukrani zangu ziwaendee watu wazuri kweli wa Jamii za Magharibi (mwa Canada) ambao nilifurahia kufanya kazi nao kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Ufafanuzi wa Phil:

Ikiwa umesoma kwa makini utagundua kuwa yamkini kuna tofauti wakati David anaposema kuwa si lazima kupata makubaliano na jamii ndipo uanzishe mradi, ili hali vifaa muhimu vya mafunzo katika tuvuti hii vinasema kuwa kuleta umoja ni kipengele muhimu katika kipindi cha uhamashishaji. Tofauti iko tu katika eneo la mradi huo. Kila jamii ni tofauti, hivyo basi mhamashishaji lazima abadilishe kipindi hicho ili kiweze kulingana na matakwa ya jamii hiyo. Vifaa vya kwanza vya uhamashishaji vilikusudiwa kutumiwa kwa vikundi vya mapato ya chini barani Afrika. Kazi ya David ililenga jamii zinazoishi kando kando ya jiji la Victoria katika magharibi mwa Canada ambazo zimeendelea kidogo (kuliko hizo za Afrika) na zina kiwango cha juu kidogo cha mapato. Katika mafundisho yetu ya uongozi na usimamizi, tunasema "Sio lazima uwe mbaya ili uwe mzuri" lakini David anatohosa hayo kwa kusema "sio lazima uwe maskini na mnyonge ndipo uwe mwenye nguvu na mwenye kujitegemea zaidi."

––»«––

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011

 Nyumbani

 Uhamashishaji