Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
YALIYOSOMWAPamoja na Hamasisho kuhusu uwezo wa kuendeleana Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Lillian Odembo NakaKifafanuzi cha mafunzoJinsi wachochezi wa jamii wanavyo kuja na kuondoka katika kila jamii,ni muhimu kuwe na kiunganishi baina yao;kile ambacho kila mmoja wao atajifunza kiwe kumbukumbu kwenye shughuli yote ya muingilioBinadamu hujifunza kutokana na kufaulu na kutofaulu, kutokana na kufanikiwa na kutofanikiwa.Kumbuka kwamba, makosa,kutofaulu na janga, yote sio sawa. Kosa, sio kutofaulu;mwanadamu hukosea.Kutofaulu sio janga; kutofanikiwa haimaanishi kuwa huwezi kufaulu. Janga halimaanishi mwisho wa maisha au mwisho wa wakati.Tunapo anguka chini, ni lazima tuamke na kuendelea mbele. Siku baada ya nyingine. Ikiwa umefanikiwa kuiongoza jamii kujijengea choo,au kukamilisha lengo fulani, basi umepiga hatua moja katika harakati ya kuifanya jamii kujitegemea.Pengine mambo hayakuwa shwari au bila dosari. Ukidhani kuwa shughuli yote haikuwa na dosari, hautakuwa mwaminifu kwa nafsi yako. Changanua harakati zote pamoja na majukumu yako. Ni muhimu uwe mkweli katika kuungama makosa yako. Andika uchanganuzi wako wa mzunguko wa uchochezi wa jamii. Kuwa na lengo bila kuegemea upande mmoja kuhusu makosa au kutofaulu; usiyatumie kama visababu vya kukudhalilisha. Yatumie kama masomo, ujifunze kwayo;yachukua kuwa ya muhimu zaidi ya yale unayoweza kujifunza kwa kusoma kwenye kitabu au kifafanuzi kama hichi. Tumia yote uliyoyandika kwenye kijitabu chako,uchanganuzi wako, na uliyojifunza ili kujikuza na kujiongezea ujuzi wa uchochezi wa jamii. Fanya vivyo hivyo pamoja na kwa niaba ya jamii. ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
nyumbani Ukurasa |
Kudhibiti muingiliano |