Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
KUDHIBITI MUINGILIANOZaidi ya muhudumu mmoja wa jamiina Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Lillian Odembo NakaUtangulizi wa kisomo (kitovu)Nyaraka zinazopatikana hapa Kudhibiti Kisomo
Huwezi kujenga misuli kwa kuinua uzani mara mojaUkitazama tena maneno muhimu na mawazo yaliyotajwa kwenye Sura ya kwanza na uyaone yenye umuhimu kwako, utakuta neno "Udhibiti." (Halipatikani kwenye kamusi nyingi). Tunawezaje kudhibiti kitu tulichoanzisha ili kiendelee kuwepo? Kwa jamii, ambayo lengo lao lilikuwa ubora wa afya, na kuchimba choo, swali lao kuu juu ya udhibiti ni, "Tutahakikishaje kuwa choo ,kitawekwa safi, kurekebishwa na kutumiwa?" Jibu ni kuhakikisha jamii imewajibika (kwa kuhusika kwenye maamuzi na udhibiti) tangu mwanzo wa mradi. Kwako wewe uliye weka harakati ya mabadiliko, kwa kuipa jamii nguvu,swali kuu juu ya udhibiti ni " Jamii itaendeleaje kushika hatamu za maendeleo yao,kufanya utathmini wa hali yao,kuchagua mambo mapya yanayohitaji kupewa kipaumbele, kutafuta rasilimali zengine, kutenda vitendo vipya, kuongeza uwezo wao wa kujitegemea?" Malengo yako na ya jamii ni tofauti, lakini yanahusiana.Unataka muingilio wako udhibitiwe. Swali la udhibiti linajibika jinsi unavyoendesha shughuli zako za uchochezi. Lengo lako sio choo,shule,zahanati au usambazaji maji kwa mara moja pekee. lengo lako ni maendeleo yaliyo dhibitiwa. Kisomo hiki kinaangazia jinsi unavyoweza kufanya kazi yako idhibitiwe.Sehemu ya jibu, lipo kwenye kurudia mzunguko wa kuiunganisha jamii kufanya jambo; sehemu nyengine ipo kwenye kutambua na kuwafunza wahudumu wa jamii kutoka kwa jamii yenyewe. ––»«––Kitendo cha manufaa;Utengezaji wa Sabuni Ukinakili
kutoka kwa tovuti hii,tafadhali muungame mwandishi |
Ukurasa wa nyumbani |