Ukurasa wa nyumbani
 Maneno muhimu


Tafsiri:

Akan
Bahasa Indonesia
Català
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
हिन्दी /   अः
हिन्दी /   ऊ
Italiano
日本語
Kiswahili
Português
Română
Srpski
Русский /   ë
Русский /   у
Русский /   ю
Tiếng Việt
Türkçe
Yoruba

                           

Kurasa nyingine:
Maneno muhimu
Visomo

Sociology:
Home Page
Lecture Notes
Discussions

Utilities:
Ramani ya tovuti
Wasiliana nasi
Nyaraka za matumizi
Tovuti zinazohusiana


Viungo vya maneno yanayoanza na herufi:

  A   B   Ch   D   E   F   G   H   I   J   K   L   M   N   O   P   R   S   T   U   V   W   Y   Z


Maneno muhimu U, ya maendeleo ya jamii, uwezeshaji na ushiriki

Mwandishi Phil Bartle

Mtafsire: Alpha Mukama, Abdulrazzaq Adam Otieno


Udhibiti

Neno "Udhibiti" ni muhimu kwa usaidizi wa kimaendeleo. (Neno lenyewe halipatikani kwenye kamusi nyingi za kiingereza). Linaashiria "uwezo" wa kitu "kudhibitiwa" (kuendelezwa) baada ya kuondolewa kwa msaada kutoka nje. Kwa jamii yenye mradi wa kusambaza maji: kurekebisha,kusafisha na kutumia pampu baada ya ujenzi ndiyo haja yao kubwa.

Kwa Mfadhili,ni kuendelea kwa mradi baada ya yeye kujitoa. kwako wewe mchochezi wa jamii, haja yako kuu ni kuendelea kwa shughuli za kuiboresha jamii utakapoondoka. Kwa wanamazingira na wanaekologia, haja yao kuu ni kwamba kitendo kidhibitiwe (kwa mfano; kibiologia) na mazingira na kwamba rasilimali zisizoweza kufufuliwa hazitatumiwa kwisha.

 العربيّة الاستمرارية,    Bahasa Indonesia: Keberlangsungan,    Català: sostenibilitat,    Deutsch: Nachhaltigkeit, die nachhaltigkeit,    Ελληνικά: Bιωσιμότητα,    English: sustainability,    Español: sostenimiento,    Filipino: maipapatuloy,    Français: durabilité,    हिन्दी (Hindi): निरंतरता,    Italiano: sostenibilita,    日本語: 継続,    Kiswahili: udhibiti,    Português: sustentabilidade,    Română: dezvoltare durabila,    Pyccкий: устойчивость,    Somali: xejin,    Srpski: održavanje,    ไทย: ความยั่งยืน,    Tiên Việt: Tạm dịch là sự phát triển bền vững,    اردو (Urdu): سسٹينيبِلٹ, سسٹينيبِلٹی"    中文 / Zhōngwén: 持续性


 

Ugomvi wa kitabaka

Hii ni dhana iliyotumiwa na Karl Marx, katika jamii za kiviwanda, na ugomvi kati ya wenye navyo na wasio navyo (wanaouza nguvu zao kwa wenye navyo ili waweze kuishi).

Katika jamii yako kama mwezeshaji katika jamii wa wakulima, utawaona wenye navyo katika uzalishaji kama wamiliki ardhi (kama ilivyo kabla ya viwanda) na wakulima, vibarua au manamba.

Katika jiji kama mwezeshaji hutaona mwenye nacho yoyote anayemiliki viwanda au mali, ila utaona wafanyakazi na wapangaji katika makazi ya hali ya kipato cha chini.

 Català: lluita de classes,    Deutsch: klassenkampf,    Ελληνικά: μαχη ταξεων,    English: class conflict,    Español: lucha de clases,    Français: conflit de classe,    Italiano: lotta di classe,    Kiswahili: ugomvi wa kitabaka,    Português: conflito de classe,    Pyccкий: классовое противоречие,    中文 (Zhōngwén): 阶级冲突


 

Uhodari

Uhodari ina maana ya ushujaa, Na niushujaa si kwa kufanya jambo gumu bali kwa kulifanya kiusahihi, kama vile kuwa mwaminifu na muwazi katika pesa za kikundi au jamii.

Pia ni chanzo cha neno "tia moyo", kituambacho wewe kama mwezeshaji utakuwa unajaribu kukifanya, kuwasisimua ili waache uchoyo na ubinafsi na wajiingize zaidi katika kazi za kuisaidia jamii na jinsi kiongozi mzuri anavyotakiwa kuwa.

 Català: coratge,    Deutsch: mut,    Ελληνικά: κουράγιο,    English: courage,    Español: ánimo,    Français: courage,    Italiano: coraggio,    Kiswahili: uhodari,    Português: coragem,    中文 (Zhōngwén): 勇气


 

Ujinsia

Neno "ujinsia" linatumika katika kutofautisha aina mbili za maneno "kiume" na "kike."

usichanganye na neno " jinsia" ambalo linatumika katika kutofautisha "mwanaume" and "mwanamke."

Ujinsia na namna ya kutafsiri nini maana ya kiume na kike inatofautiana kati ya tamaduni na tamaduni, na kati ya jamii na jamii.

Nia yetu kuhusu ujinsia ni kuona jinsi gani inaweza kuathiri mgawanyo wa madaraka, uhusiano kiuchumi, na tofauti za kijamii.

Hii ni mojawapo ya jambo muhimu linaloathiri jamii na pia linaathiri kazi ya mwezeshaji.

Mwezeshaji lazima (pia ni moja ya hitaji la kusoma kuhusu jamii) kuelewa thamani, muelekea na maadili yanayoizunguka jamii husika.

Mwezeshaji pia anafanya kazi katika kupunguza tofauti iliyopo kisiasa na kiuchumi kati ya jinsia, kama kiungo muhimu katika uwezeshaji. Angalia moduli ya ufundishaji Ujinsia.  Ujinsia Umri, Rangi, na Jinsia.

 বাংলা : লিঙ্গ,    Bahasa Indonesia: gender,    Català: gènere,    Deutsch: gender,    Ελληνικά: γένος,    English: gender,    Español: género,    Euskera: generoa,    Filipino/Tagalog: pangkasarian o kasarian,    Français: genre,    Galego: xénero,    Italiano: genere,    日本語: ジェンダー,    Kiswahili: ujinsia,    Malay: gender,    Português: género,    Română: gen,    Somali: Jandar,    Tiên Việt: giới tính,    Türkçe: toplumsal cinsiyet,    中文 (Zhōngwén): 性别问题


 

Ukarabati wa kijamii

Ukrabati hapa unamaanisha mazingira (kibaiolojia), hisia au kiakili (au urudishaji) wa watu ambao wameathirika kiuwezo kimwili, kimawazo au kiakili.

pale ambapo ukarabati ni wa kijamii basi maamuzi yote na majukumu ya wakuwasaidia wote walioathirika ni ya jami na hayaanzii nje ya jamii.

Angalia ufupisho, CBR.


 

Uongozi

Neno Neno ni neno pana zaidi ya neno serikali.

Si rasmi na inahusisha zaidi sheria katika maana yake.

Inamaanisha namna nzima ya kufanya maamuzi, menejimenti ongozi, uratibu na nguvu ya uongozi katika muundo wowote kama jamii.

Uongozi bora ni uaminifu ushirikishaji, uwajibikaji, uwazi, uendelevu, usawa, demokrasia, kuheshimu watu wote na kuwatumikia.

 Català: governament,    Deutsch: Regierungsführung,    Ελληνικά: διοικηση,    English: governance,    Español: gobierno, administración,    Français: gouvernance,    Italiano: governance,    Kiswahili: uongozi,    Português: governação,    Română: guvernanță,    Somali: hogaanka,    Türkçe: yönetim,    中文 (Zhōngwén): 管治


 

Ushiriki wa jamii

Ushiriki wa jamii ni ziadi ya kuchangia pesa, au nguvu ya kazi, au vifaa, ni kushiriki katika kufanya maamuzi kuchagua mradi wa jamii, kupanga, kutekeleza, kutawala, kudhibiti, na kuongoza. inatofautiana na mchango wa jamii.

Ramsa ya kijamii inaendeleza shughuli za jamii huku ikiwa katika nafsi ya jamii kuchukua majukumu zaidi kwa maendeleo yake, kuanzia maamuzi ya mradi upi wauchukue na kuangalia namna ya kukusanya mali ghafi kwa ajili ya mradi husika.

ushirikishwaji wa jamii unahakikisha kuwa maamuzi yanayo husu mradi yanafanywa na wanajamii wote. (sio wachache) au watu toka nje.

Katika njia hii, mchango wa jamii unasaidia watu kujisitoa kwa hali na mali katika mradi sababu wanaushirika nao. PIa tunazishauri serikali na wafadhili wake kuzihusisha jamii husika katika kupanga miradi yao.

Ushirikishwaji wa jamii hapa usichukuliwe kama mbadala wa michango ya jamii. (kama inavyofanywa na watu wengi kimakosa); Ushiriki hapa una maanisha kushiriki katika kufanya maamuzi, kuongoza na kuchunga.

 বাংলা : জনগোষ্ঠির অংশগ্রহন,    Bahasa Indonesia: peran serta masyarakat,    Català: participació comunitària,    Deutsch: gemeindepartizipation,    Ελληνικά: κοινοτική,    English: community participation,    Español: participación comunitaria,    Euskera: komunitatearen parte-hartzea,    Filipino/Tagalog: pakikilahok ng komunidad,    Français: participation de la communauté,    Galego: participación comunitaria,    Italiano: partecipazione della comunità,    日本語: 共同体の参加,    Kiswahili: ushiriki wa jamii,    Malay: penyertaaan komuniti,    Português: participação da comunidade,    Română: participarea comunitatii,    Af Soomaali: ka geyb galka bushada a,    Tiên Việt: sự tham gia của cộng đồng,    Türkçe: toplumsal katılım,    中文 (Zhōngwén): 社区参与


 

Ushupavu

Ushupavu ni moja ya elementi kumi na sita za nguvu, uwezo, au nia ya jamii au ushirika. Angalia: ELementi za nguvu ya jamii.  ikiwa inasilishwa kibinafsi ni kiasi gani watu wanashiriki katika ushupavu kama jamii.  mfano katika kuamini kuwa jamii inaweza kupata/ kufanya jambo fulani.

mitizamo chanya, nia, ushawishi binafsi, mshawasha, maono, kujitegemea na si utegemezi, nia ya kupigania haki, kutokuwa wabinafsi na wachoyo, na maono ya nini kinawezekana. Kuongezeka nguvu inamaana ya kuongezeka ushupavu.  Unapokuwa unaihamasisha jamii kufanya jambo fulani, mwezeshaji unatakiwa kufahamu kazi ya ushupavu katika kuiwezesha jamii au ushirika.

 Català: confiança,    Deutsch: zuversicht,    Ελληνικά: εμπιστοσυνη,    English: confidence,    Español: confianza,    Français: confiance,    Italiano: sicurezza,    Kiswahili: ushupavu,    Português: confiança,    中文 (Zhōngwén): 信心


 

Usugu

Usugu ni moja ya aina tano za umasikini na utegemezi

Wakati mwingine huhusihwa na filosofia ya kifo Muombe Mungu lakini pia jisaidie" kwa kirusi msemo, unasema kuwa tuko kwenye mikono ya Mungu, lakini pia tuna majukumu yetu binafsi.

Tumeumbwa na uwezo mwingi: kuchagua, kushirikiana, kupanga, na kuinua viwango vya maisha yetu; tusimtumie Mungu kama njia ya kukwepa kufanya kazi.

 العربيّة: العربيّة,    বাংলা : উদাসীনতা,    Bahasa Indonesia: apatis,    Català: apatia,    Deutsch: Apathie,    Ελληνικά: απαθεια,    English: apathy,    Español: apatía,    Euskera: apatia,    Filipino: pagsasawalang bahala,    Français: apathie,    Galego: apatía,    हिन्दी : बेपरवाही,    Italiano: apatia,    日本語: 無関心,    Kiswahili: usugu,    Malay: apati,    Português: apatia,    Română: apatie,    Pyccкий: апатия,    Somali: naceyb,    Tiên Việt: sự thờ ơ,    Türkçe: duyarsizlık,    中文 : 态度冷淡


 

Utamadunisho

Neno "utamadunisho" ni jinsi au namna ya kujifunza utamaduni mpya, tofauti na enculturation.

mara nyingi humaanisha kwenda kwenye jamii mpya ambapo tamaduni ni tofauti, lakini pia ni sehemu ya mazoea ambayo tunayahitaji kwa ajili ya kuzoea mabadiliko katika jamii zetu (nina maana ni endelevu) zinazotuzunguka.

Kazi yako kama mwezeshaji itatoa matokeo ya mabadiliko ya jamii ( maendeleo)katika jamii. wanachama kwenye hiyo jamii ni lazima"wajitamadunishe" (wajizoeshe) kwenye jamii mpya.

Angalia majadiliano ya wanafunzi katika maingiliano (socialization).

 Català: aculturació,    Deutsch: akkulturation,    Ελληνικά: εκπολιτισμοσ,    English: acculturation,    Español: aculturación,    Français: acculturation,    Galego: aculturación,    हिन्दी : उत्संस्करण,    Italiano: acculturazione,    日本語: 文化変容,    Kiswahili: utamadunisho,    Português: aculturação,    Română: aculturarea,    Pyccкий: аккультурация,    Türkçe: kültürleşme,    中文 : 文化适应


 

Utawala binafsi

"Utawala binafsi"ni neno lilitokana na neno la kihispania toka Marekani ya kusini na kati, "Uongozi binafsi." Ina maanisha jamii kujitawala yenyewe. Angali Binafsi.

Angalia Utawala binafsi. Inamaanisha kuwa jamii imechukua hatamu kwenye utawala na katika kufanya maamuzi yatakayoleta maendeleo.

 Català: auto gestió,    Deutsch: selbstverwaltung,    Ελληνικά: αυτοδιαχειριση,    English: auto management, self management,    Español: autogestión,    Français: auto gestion,    Galego: AUTOXESTIÓN,    हिन्दी : स्वचालित प्रबंधन,    Italiano: autogestione,    日本語: 自主管理,    Kiswahili: utawala binafsi,    Português: auto gestão,    Română: auto management,    Pyccкий: автоменеджмент,    Türkçe: otoyönetim,    中文 : 自行管理


 

Uwezeshaji wa jamii

Kuongeza uwezo wa jamii kuongeza uwezo wake wa kufanya jambo.

Ni zaidi ya kuongeza kazi ya kijamii, au huduma ya kijamii kama barabara, maji, elimu na huduma za afya.

kuongez auwezo na nguvu.inamaana stadi na maarifa zaidi na kuw amakini zaidi. haiwezi kuja kwa bahati au michango y amali ila kwa kuwezeshwa kupitia miradi ya kijamii, ila tu endapo wanajamii watahusishwa tokea mwanzo.

Kuongeza demokrasia kutaisaidia serikali katika utawala na kuachia sehemu ya kutunga sheria kwenda kwenye jamii, mfano kufanya maamuzi juu ya maendeleo yake binafsi,-nguvu, uwezo nia. uwezeshwaji¨

বাংলা : জনগোষ্ঠির ক্ষমতায়ন,   Bahasa Indonesia: pemberayaan masyarakat,   Català: potenciació comunitària,   Deutsch: gemeindestärkung,   Ελληνικά: κοινοτική ενδυνάμωση,   English: community empowerment,   Español: potenciación comunitaria,   Euskera: komunitatea sendotzea,   Filipino/Tagalog: pagsasakapangyarihan ng komunidad,   Français: fortifier de la communauté,   Galego: potenciación comunitaria,   Italiano: potenziamento comunitario,   Kiswahili: uwezeshaji wa jamii,   日本語: 共同体強化,   Malay: pemberdayaan komuniti,   Português: fortalecendo da comunidade,   Română: consolidarea coomunitatii,   Tiên Việt: sự uỷ quyền cộng đồng,   Türkçe: toplumu güçlendirme,   中文 (Zhōngwén): 强化社区


 

Uwezo

Nia, nguvu au ushupavu wa jamii au ushirika.

 العربيّة: قدرة,    বাংলা : সক্ষমতাঃ,    Bahasa Indonesia: kapasitas,    Català: capacitat,    Deutsch: Macht, empowerment, die stärkung, leistungsfähigkeit,    Ελληνικά: δυνατότητες, ισχύς, δύναμη,    English: capacity, power, strength,    Español: capacidad, potenciación,    Euskera: gaitasuna,    Filipino/Tagalog: kakayahan, pagpapalakas,    Français: capacité, empowerment,    Galego: capacidade,    हिन्दी (Hindi): क्षमता,    Italiano: empowerment,    日本語: 容量, 強くする,    Kiswahili: uwezo,    Malay: kapasiti,    Português: capacidade, fortalecendo,    Română: capacitate,    Pyccкий: paзвития,    Af Soomaali: awooda,    Tiên Việt: năng lực, tăng cường,    Türkçe: kapasite,    中文 (Zhōngwén): 能力


──»«──
Kama umeona neno linalohusiana na uwezeshaji jamii na unataka kujadili, tafadhali tuandikie.
kama utanakili maandishi kutoka kwenye mtandao huu, tafadhali mnukuu mwandishi au waandishi
na ufanye marejesho www.cec.vcn.bc.ca
This site is hosted by the Vancouver Community Network (VCN)

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Ukurasa umesanifiwa na Lourdes Sada
──»«──
Imehakikiwa: 2015.10.14


 Ukurasa wa nyumbani