Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
KUUDHIBITI MZUNGUKO KATIKA MRADI WA MAENDELEOMradi mmoja wa kijamii ni mwanzo tuna Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Lillian Odembo NakaKifafanuzi cha mafunzoKila muingiliano,kila mzunguko katika kutendeka kwa mradi, Kila mradi wa kijamiii, unachangia katika kuiwezesha jamii; Lazima mzunguko huo urudiwe kila maraHapo awali, kazi yako,jukumu lako kwa jamii, Ilikuwa kama kisababisho cha maendeleo katika jamii.Vitendo vyote, (kutathmini hali ilivyo,kuhamasisha jamii, kuimarisha umoja ,(kupanga na kutekeleza mipango,kisha kutathmini hali kwa mara nyingine) ni kama changamoto cha kuimarisha jamii na kuipatia nguvu za kujitegemea "Neno mzunguko" laweza kuwa la kutatanisha hapa. Kwa hakika,ufikapo mwisho utarudia mwanzo tena, lakini kwa mara hii, wewe pamoja na jamii mumebadilika. Msemo wa kibudhisti (Budhist) husema kwamba," Mtu yuyo huyo hawezi kuvuka mto huo huo mara mbili,"(mtu na mto hubadilika kila mara) Hata hivyo, ni muhimu kurudia vitendo muhimu ili kuhimiza maendeleo katika jamii.Gurudumu la baisikeli linapovurumishwa, kila sehemu ya gurudumu hilo hugusa sehemu tofauti ya barabara kila mara lizungukapo. Hata hivyo, usisahau kwamba wakati ukifika utaicha jamii hiyo, kumbuka jambo hili tangu mwanzo wa majukumu yako.Ikiwa jamii hiyo haiwezi kuendelea bila wewe, basi imekutegemea. Adui yako ni kutegemewa. Unaporudia mzunguko huo wa mradi, nia yako ni kujitoa ili mzunguko huo uendelee bila wewe.Ukipata mrithi wa majukumu yako ,yale yote uliyoyaandika kwenye kijitabu chako, tangu sura ya kwanza yatakusaidia wakati unapoukabithi wadhifa wako kwa mtu mwengine. Ikiwa shirika lako halitatuma mtu wa kukurithi, lazima ujitafutie mtu atakaye chukua majukumu yako katika jamii. ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
nyumbani Ukurasa |
Kudhibiti muingiliano |