Tafsiri:
Kurasa nyingine:
Yaliyomo:
Yaliyomo:
|
KUCHANGIA MAWAZO; TARATIBU NA MTINDO
imetafsiriwa na Lillian Naka
Utaratibu wa mbinu
Mbinu katika matayarisho ya uwezeshaji wa jamii
Mwongozo
huu utakuwezesha kukisaidia kikundi kufanya uamuzi kwa pamoja.Mbinu hii yaweza kutumika
kwenye mkutano wa kijamii,mkutano wa viongozi wa shirika la kijamii,viongozi wa mashirika
yasiyo ya kiserikali,shirika la kiserikali au shirika la umoja wa mataifa, kati ya
washiriki watano hadi mia mbili.
Maadamu
una ujuzi wa kukiongoza kikao na utahakikisha mtindo na kanuni za kikao zimefuatwa
(kwa mfano, hakuna kukosoa au kumsuta mwengine), utakuwa unahakikisha kuwa maamuzi
ni ya kundi zima na wala hayakulazimishwa na uwepo wako.Utakuwa una sahilisha uamuzi
wa kundi.
Madhumuni
ya kikao cha kuchangia mawazo:
Madhumuni
ya kikao cha kuchangia mawazo ni kutambua shida na kutafuta kwa pamoja, uamuzi mwafaka
wa kutatua shida hiyo.
Mahitaji;
- Shida inayohitaji kutatuliwa;
- Kikundi chenye uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja.Hii hutumika kwa kundi la watu wapatao watano
hadi kumi (kwa mfano wafunzi,shirika la wafanyikazi,wanaofanya kazi nje ya ofisi
zao), hadi mkutano wamamia ya wanakijiji;
- Ubao,kurasa za karatasi kubwa au kitu ambacho kitaonekana vyema na wote, na kalamu zenye maandishi
manene;na
- Msahalishi(wewe).Mtu ambaye jukumu lake ni kuandika vidokezo vya washiriki wala si maoni yake,na utumie
ujuzi wa uongozaji kudhibiti nidhamu na malengo ya kikao.
Kanuni za kimsingi:
- Msahalishi ataongoza kila kikao;
- Msahalishi ataalika washiriki kutoa vidokezo;
- Hakuna kukosoa (dokezo la mwengine);na
- Vidokezo vyote viandikwe ubaoni (hata vile visivyostahili)
Taratibu:
- Fasili au tambua shida:
- Uliza vidokezo juu ya shida muhimu;
- Hakuna kukosoa dokezo la mwengine;
- Andika shida zote zilizodokezwa ,ubaoni
- Ziweke pamoja, shida zinazoambatana au kuhusiana;kisha
- Ziandike upya kulingana na umuhimu (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
- Zalisha Lengo:
- Pindua fasili ya shida (suluhisho lake)
- Suluhisho la shida iliyofasiliwa hapo juu, ndilo lengo
- Fasili lengo kama suluhisho la shida;
- Andika lengo hilo ubaoni; kisha
- Likumbushe kundi kwamba lengo hilo ndilo walilo chagua
- Fasili Nia au shabaha:
-
- Elezea tofauti kati ya shabaha au Nia na Lengo;
- Msahalishi anastahili kufahamu haya:(Tazama HODARI;Shabaha, yaweza kukadiriwa,ina kiwango na tarehe ya kumalizika).
- Uliza kundi litoe vidokezo kuhusu shabaha;
- Andika vidokezo vyote kuhusu shabaha, Ubaoni;
- Hakuna anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mtu yeyote);
- Viweke pamoja, vidokezo vinavyohusiana au kuambatana;
- Viandike upya kulingana na umuhimu wake (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
- Wakumbushe washiriki wa kundi kuwa, ni wao, waliozalisha shabaha hizo.
- Tambua rasilimali na vizuizi:
- Uliza kundi litoe vidokezo kuhusiana na rasilimali na vizuizi;
- Viandike vidokezo vyote kuhusiana na rasilimali na vizuizi, ubaoni;
- Hakuna anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mshiriki yeyote);
- Ziweke pamoja rasilimali zinazofanana au kuhusiana.
- Ziandike upya kulingana na kipaumbele (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
- Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
- Viweke pamoja , vizuizi vyote vinavyofanana au vinavyoambatana.
- Viandike upya kulingana na kipaumbele(vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
- Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo.
- Tambua mbinu:
- Uliza kundi litoe vidokezo kuhusu mbinu zitakazotumika;
- Viandike vidokezo vyote ubaoni;
- Hakuna apaswaye kukosoa (kidokezo cha mwengine)
- Viandike pamoja, vidokezo vinavyoambatana au vinavyohusiana ;
- Viandike upya kulingana na kipaumbele (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);
- Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
- Chagua mtindo ulio juu ya orodha.
- Andika ubaoni, maamuzi ya kundi kwa ufupi:
- shida;
- lengo;
- shabaha au Nia;
- rasilimali
- vizuizi; na
- mtindo;
Elezea
kundi kwamba, wametengeza mpangilio wa vitendo vitakavyotumika. Ikiwa mtu ataandka
yaliyoamuliwa katika kila kitengo kilichotajwa hapo juu,atapata kiini cha waraka
wa mpangilio.Waeleze kwamba,wametayarisha mpango huo kwa pamoja na "wanaumiliki".
Mwisho:
Ni
nyepesi.Hii haimaanishi kuwa ni rahisi lakini huboreka ikiwa desturi.kwenye kila
sehemu ya kikao hicho,waweza tumia michezo ya kuigiza,michezo inayojumuisha kundi
na mbinu zengine.Jaribu mitindo tofauti mara kwa mara.
Heri
njema na mafanikio kwenye uchochezi wa jamii!
––»«––
Maamuzi
kwenye mfano huu yametokana na maswali
yale manne ya msingi kuhusu
usimamizi.Majibu ya maswahili hayo, ,kwa pamoja, ndio kiini cha ushauri
wa mradi.Kama
njia mbadala,kikao cha SWOT chawezatumika
kwa kundi kubwa.
Kikao cha kuchangia mawazo:
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Web Design: Lourdes Sada
––»«––Imeratibishwa mwisho: 08.11.2011
|