Ukurasa wa nyumbani
Tuanze mada




Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Български език
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Euskara
Ewe
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
한국어 / Hangugeo
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Português
Română
Русский
>తెలుగు /Telugu
ไทย / Thai
Türkçe
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

KUIMARISHA KWA KUPANGA

Kuongeza Uwezo kwa Kupanga

Na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Jacob Lisakafu


Nakala ya Kufundishia

Sababu nyingine zitakuwa sawa, Uimara utategemea level ya kupanga

Kuna sababu nyingi zinachangia kwa uimara, uwezo au uwezeshaji, Kitu kimoja muhimu kwa mhamasishaji ni "kupanga."

Sababu nyingine ni sawa, ukubwa wa ufanisi wa taasisi unaweza kuonyesha uimara wa kikundi, wakala au jumuia.

Tunaweza kutumia timu ya mpira wa miguu kama mfano.Kama una timu mbili za mpira wa miguu, zenye namba sawa za wa wachezaji,uwezo sawa, kuwa imara kimisuli, na ufundi (kwa mfano uimara viatu), unaweza kuwa sawa. Timu mmoja haijajipanga; hakuna mganwanyo wa kazi, hawana mfumo mzuri.Na timu nyingine imejipanga vizuri, wana mwalimu mwenye mamlaka, wana sheria tofauti za magolikipa,walinzi,mawinga wa pembeni, kiungo mshambuliaji, na mgawanyo mwingine wa wafanyakazi.

Sababu nyingine zinaweza kuwa sawa, Uimara unategemea level ya kujipanga au kupanga. Timu tofauti wana majukumu mbali mbali na kucheza katika hali inayoeleweka (kupeana mipira). Katika kesi hii, ni rahisi kuona timu ya pili ina nguvu zaidi,ni imara zaidi na ina uwezo kuliko timu ya kwanza, japokuwa wanalingana kwa tabia nyingine.

Upangaji bora unaweka uwezo mkubwa. Sawa na jamii zote.

Chukua mfamo huu (sio kwa kihistoria bali kwa kanuni za kisaikologia ). Akan of West Africa walijitanua kwa kasi kipindi cha karne ya kumi na sita na kumi na saba, na kwa haraka waliteka Waguans waliowaachia wao. Uwezo wa kiufundi (ukijumuisha silaha) zilikuwa sawa, na kama tabia nyingine.

Lakini Waguan walikuwa wanarithi ardhi na ukoo wao unatoka kwa baba waliishi mbali mbali kifamilia, Wakati waakani walikuwa wanarithi ardhi na ukoo wao unatoka kwa mama na kukusanya familia mbali mbali na kuwa chini ya uongozi mmoja, waliishi kwenye makazi ya pamoja, kila familia ilikuwa na majukumu mbali mbali kwenye vita (kwenda mbele, pembeni, nyuma, nyumbani na kwenda juu) na kuipanga utawala wao.

Kama katika kupanga timu ya mpira, sababu nyingine zinabakia kuwa sawa (ufundi na uwezo),Jamii iliyojipanga vizuri (waakani) waliweza kuteka jamii zisizo jipanga vizuri.

Arama , kama wewe ni muamasishaji,lengo lako liwe ni kiumarisha jumuia yenye kipato kidogo, kusaidia kupata kikundi cha walengwa kilichopangwa vizuri na kwa ufanisi.

Usiunde au usianzishe CBO. Utendaji uwe chini yao, au wasaidie kuchagua mwenyekiti, makamu, katibu mustasi, na mweka hazina, wasaidie kupata uongozi, kupata mfumo mzuri, au kupanga kwa kupata ufanisi zaidi, kuwaajiri wao.Kupanga bora matokeo yake ni kupata utawala wenye nguvu.

Visomo vingine vitakuongoza kupanga. Kuwa makini kwa nini unapanga (na mwisho wapi) na wafanye kikindi kilengwa kishiriki kama rafiki katika kuiwezesha jumuia yenye kipato kidogo.

––»«––

Kujipanga kwa Jumuia


Kujipanga kwa Jumuia

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 12.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Tuanze mada