Ukurasa wa Nyumbani
Matayarisho




Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
বাংলা / Baṅla
Български език
Català
Cebuano / Sugboanon
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Euskara
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
ગુજરાતી / Gujarātī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Português
Română
Af Soomaali
తెలుగు /Telugu
Tiếng Việt
Türkçe
Èdè Yorùbá

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

KUMUANDAA MRATIBU

Mwongozo wa Mkufunzi

na Phil Bartle, PhD

Imetafsiriwa na Elie Chansa


Kitini cha Mkufunzi

Kutumia modul hii kwa kufundishia

Nani Anaweza Kuwa Mwanaharakati wa Jumuiya?

Siyo kila mtu ni mratibu mzuri wa jumuiya.

Hata hivyo, usichukulie ya kwamba, mafunzo ama elimu katika masomo fulani yatakuhakikishia upendeleo wa kufanya kazi na jumuiya. Cheti au diploma ya kazi za ustawi, ama masomo husika hayatamfanya mtu kuwa makini katika kukuza jumuiya zenye kipato kidogo. Wahandisi, wahitimu wa biashara au sayansi, na hata wale walio mwaka wa kwanza wa mosomo yao, wote wamekuwa wafanyakazi wa jumuiya tena kwa umakini mkubwa.

Kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo, kuwa mfanyakazi wa jumuiya, kunahitaji mchakato wa uchaguzi binafsi.

Kama unawafunza waratibu watarajiwa, inabidi upange mipango katika namna ambayo itakuwa rahisi kwa walio mafunzoni kuchagua njia mojawapo.

Modul hii kuhusu matayarisho, ina zana ambazo unaweza kutumia kuwawezesha waratibu wenye uwezo kwenye asili ya kazi zao, tabia binafsi wanazohitaji na mafunzo gani ambayo watakutana nayo. Itumie kutengenezea mazingira ili kwamba wafanye maamuzi kama wataendelea na mafunzo.

Zana za awali za kufundishia:

Modul tano za awali kwenye mtandao huu, katika mafunzo haya, zina haswa vitini vichache, mahsusi kutumika kwenye kongamano za mafunzo, na inabidi zijadiliwe na kueleweshana polepole na pia kidogokidogo. Zote zinategemea yaliyomo kwenye kijitabu cha kwanza cha maelezo, ambacho kimewasilishwa kama kitu kamili sehemu nyingine kwenye mtandao huu.( Kijitabu cha Mratibu). Kimetenganishwa katika vitini vifupi tofauti ili kipate kutumika tofauti kwa ajili ya majadiliano kwenye kongamano.

Unaweza kuwashauri wanafunzi wapitie kijitabu hicho kama watataka kusoma hati ndefu inayohusisha zana zote.

Modul za baadae zina hati ndefu na pia zenye mambo yenye ujuzi zaidi.

Kila kitini kinaweza kutumika kwenye mafunzo ya dakika arobaini (kwa kutumia jina hilohilo kwenye kipindi) kwenye kongamano la mwanzo. Unaweza kuvitumia hivyo vichwa vya habari unapopanga mafunzo yako.

Ukianza na vianishi kamili kwenye Ramani ya Mtandao, Unaweza kuainisha vipindi vyako vya mafunzo katika mpangilio kama inavyoonekana kwenye modul tano za awali, ama zipangilie kulingana na mahitaji yako pamoja na ya wanaofundishwa.

Unaweza pia kunakili kila kitini, ama baadhi ya chaguzi zako, na kuonyesha kupitia mitambo, na kuionyesha kwenye skrini, ili kurahisisha maonyesho, majadiliano, na ushiriki. Ni juu yako mwenyewe kuamua jinsi gani ya kutumia hizo zana.

Tunashauri kila kipindi kihusishe zaidi njia ya washiriki "kutenda", ila njia ya mihadhara na uwasilishwaji wa upande mmoja uwe mara chache. Unaweza kufikiria na kubuni mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya washiriki kuwa hai kwenye kila kipindi, na itakusaidia ukiandika mtiririko wa hivyo vitu ili upate kuvitumia katika vipindi vingine.

Kipi kinafanya kazi kwako, kwa vipi?

Hati zinazowiana kwenye modul nyingine:

Hati mbili zilizo kwenye modul nyingine zinaweza kuwa na msaada kama utapenda kuongezea zilizopo humu tayari.

Kwenye modul ya"Duru la Uratibu" hati ya "Kuwa Mratibu " inaweza kuwa ya msaada sana hapa. Inaweza kugawanywa kwenye vitini viwili, moja ikiainisha tabia binafsi zinazotakiwa, zikiwa zimeandikwa kama vihakikisho ambavyo mshiriki atatakiwa aangalie na kujiuliza mwenyewe kama ana hizo tabia. Nyingine ni viainishi virahisi vya kazi ambazo mratibu anategemewa kufanya kwenye mafunzo. Aidha mojawapo ama vyote vinaweza kutumika kama kitini kwenye sehemu ya "matayarisho".

kwenye modul ya "Kuwezesha Uratibu", hati ya " Maelezo ya Kazi" inatoa maelezo zaidi kuhusiana na uwezo unaotakiwa, na, kazi na majukumu yanayotegemewa.

Modul hiyo, na "Uongozi Shirikishi" vinashauri kuwa uhusiano kati ya meneja na mratibu uwe wa pamoja, na kwamba wanatakiwa kushirikiana kutengeneza maelezo ya kazi ya mratibu wao. (Bahati mbaya, siyo kila mratibu atajikuta kwenye kazi ambayo msimamizi wake anashughulikia suala la uongozi shirikishi -- hizo modul mbili zinaichochea).

Kama washiriki wanaomba zaidi ya maelezo yaliyopo kwenye vitini vya "matayarisho" basi kitini cha maelezo ya kazi kitawafaa.

Mbinu za Mafunzo:

Kuna modul kamili kwenye mtandao huu ambayo ni mahsusi kukuletea mbinu mbalimbali za mafunzo, ambazo unaweza kupata habari zake unapotumia zana hii kwa mafunzo. (Mbinu za Mafunzo)

Unapoandaa mafunzo ya awali kwenye kongamano kuhusiana na mada kama "Matayarisho," pitia modul ya "Mbinu za Mafunzo" kwa ajili ya muongozo na vidokezo jinsi ya kuandaa program ya mafunzo.

Kwenye mtandao huu na program ya mafunzo iliyopo, msisitizo upo kwenye, masomo kwa vitendo. Sote tunajifunza tofauti, kwa spidi tofauti, na zaidi kwenye nyanja moja tofauti na nyingine. Hata hivyo, kwa ujumla, tunaweza kujifunza na kuhifadhi zaidi, hasahasa maarifa, kwa kufanya kitu mbali ya kukisikia ama kwa kukiangalia tu.

Tunashauri, uachane na mbinu za kiimani za kutafuta mafunzo, na utumie mibnu na ubunifu wako kuandaa mafunzo yako, kulingana na hali na mahitaji ya washiriki na mazingira husika.

Kama unaendesha program ya mafunzo, tunashauri utuandikie na ujadili utafiti na mawazo yako. Kama una maoni, labda tunaweza kutengeneza zana mpya kwa pamoja.

──»«──

kama utanakili maandishi kutoka kwenye mtandao huu, tafadhali mnukuu mwandishi au waandishi.
na ufanye marejesho cec.vcn.bc.ca/cmp/

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Ukurasa umesanifiwa na Lourdes Sada
––»«––
Imehakikiwa: 2010.03.08

 Ukurasa wa nyumbani

 Matayarisho