Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
FAHAMU DHANA ZA MSINGITaratibu na kuwaza kufuatana na Maarifana Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Elie ChansaKitini cha MafunzoDhana na taratibu ambazo mratibu anatakiwa aeleweMaendeleo ni nini, Maendeleo ya jumuiya? Ushiriki kwenye jumuiya? Umaskini? Jumuiya? Uwezeshaji? Uwazi? Ustahimilivu? Haya maneno yamejadiliwa kwenye funguo za maneno"). Kuwa mratibu mwenye mafanikio, unahitaji maarifa machache kwenye mdahalo wa umma na kuongoza makundi kwa ajili ya vitendo. Unahitaji kujua kwa nini utumie maarifa hayo. Unahitaji kujua taratibu. Kama mlengwa wako ni jamii, basi unatakiwa kujua baadhi ya dhana za kisaikolojia kuhusiana na asili ya jumuiya na asili ya mabadiliko ya kijamii (ikiwemo maendeleo) ya jumuiya. Hii inamaanisha kuwa unahitaji uelewa wa jamii shiriki, maliasili na maendeleo, asili ya watu, uchumi, siasa, na nguvu pamoja na mchakato unaohusiana na taaluma hiyo. (Tazama "Tamaduni.") Kwa sasa hakuna ulazima wa kuwa na shahada ya chuo kikuu, lakini unatakiwa ujifunze taratibu na maarifa ya masomo hayo. Ukitaka kukuza (kuwezesha ) jamii ya kipato cha chini, unatakiwa umuelewe adui, ambaye ni tatizo sugu la utegemezi. (Tazama: "Utegemezi"). Kama lengo lako ni kuondoa ama kukomesha umaskini unahitaji kujua zaidi ya dalili na matokeo ya umaskini. Unahitaji pia kuelewa chanzo cha umaskini, ili kuunga mkono, na kuchangia mabadiliko yatakayopambana na sababu hizo. Unatakiwa ujue kuwa mbinu za kupunguza umaskini zinapunguza makali kwa muda tu, ila hayachangii kukomesha umaskini. Umaskini siyo suala la hela, na hela pekee hazitokomesha umaskini (Tazama "Mbinu za Kupunguza Umaskini"). Kama ukitazama "Funguo za maneno," Utapata listi nzuri tu kuhusu dhana za msingi kuhusiana na mfanyakazi wa jamii. Kati ya zote, hutopata maana ya kamusi; utapata baadhi ya maelezo kuhusiana na makusudi ya kijitabu hichi: Jinsi ya kuwa mratibu Modul ya hivi karibuni Taratibu za kuiwezesha Jumuiya, Itakuonyesha kiundani zaidi taratibbu zinazokuwa nyuma ya mbinu na maarifa ambayo yapatikana kwenye mtandao huu. Usikariri hayo maneno. Fikiri kuhusu kila dhana. Andika kuhusu dhana hizo kwenye jarida lako Jadili na wenza katika mikutano, midahalo, ama kwenye mafunzo. Kwa muda wako unapokuwa umepumzika, baada ya kazi na marafiki, ondoa muda kidogo wa kujadili matokeo ya mpira na badala yake ujadili dhana mojawapo, au zaidi. Kujaribu kujifunza "mara moja tu na kuacha" , ni sawa na kujaribu kula "mara moja tu na kuacha" Kujifunza, kama maendeleo ya jamii, hakutakiwi kuisha. Unapoacha kujifunza, umekufa. ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Ukurasa wa nyumbani |
Matayarisho |