Tweet Tafsiri:
'العربية / al-ʿarabīyah |
JUA LENGO LAKOUnataka Kutimiza Nini?na Phil Bartle, PhDImetafsiriwa na Caroline RonoVitoleo vya mafunzoKusudi na shabaha ya kuwa MhamasishiMoja wapo ya misemo ambayo tunatumia tunapo funza ukurungenzi ni, "Kama hujui unapoelekea basi utapita popote pale." (Tazama "Misemo"). Hii pia inatumika unapo jitayarisha kuwa mhamasishaji. Ni rahisi kuelekea huku na kule ukionekana kwamba unafanya kazi mingi,ukiandaa mikutano,kuhakikisha nyuwa zimejengwa,kuongea na kuandaa mikutano na wazee wa kijiji, kuongoza vikundi vya utetezi, kuchechemua vitendo ,bila ya kuendelea mbele kusudi kuendelesha jamii dhabiti . Kwanza unastahili ujue lengo lako binafsi kisha, kwa maandishi,ya wale walio karibu nawe. Hapa,unastahili kuanza kwa kuandika katika shajara yako ama kitengo ulichoweka kando kwa kusudi ya kunukuu lengo na dhamira. Unafaa kuyachukulia kama lengo yako binafsi bali sio tu kama maadili ya mtu mwingine. Lengo la uhamasishaji ili kuendelesha jamii linaweza kubadilika kutoka mtu mmoja hadi mwingine au pia kulingana na jamii tofauti. Hata hivyo, kuna mambo yanayo lingana. Miongoni ambazo ni: Kumaliza umasikini, kuwa na uongozi bora, mabadiliko katika vitengo vya jamii, kuendeleza kadiri ya jamii, kuhamasisha maskini na watu waliotengwa, na kusawazisha jinsia. Unapoendelea kusoma kitoleo hiki na kujulisha watu wengi,utagundua ya kuwa lengo haya yanaendelea kuwa ya kuvutia na pia yenye changamoto kubwa aghalabu unapozidi kuelewa. Rudi kwa shajara yako mara kwa mara ili uweze kusashisa,kuendeleza na pia kuongezea vipengele kwa lengo unazo. Kwa mfano kupunguza umaskini ni changamoto kubwa unapo jaribu kurekebisha kuliko tu kuiandika chini.Tunajifunza kuzuia "kuongeza umaskini" kwa sababu kuandika inaondoa uchungu na wasiwasi lakini haileti suluhisho la kudumu Umaskini sio tu kukosa pesa (kama utakavyo gundua baadaye ukiendelea kusoma vitoleo hivi ) .Ili kukabiliana na mambo yanayoleta umaskini tunafaa kupigana na utepetevu, ujuhula, ugonjwa, na uongo. Huu tu ni mojawapo ya mifano ya umuhimu na manufaa inayoletwa unapozidi kuelewa lengo na kupata ufasiri zaidi Vilevile, kuwa na uongozi mwema haumaanishi tu kuwa na kiongozi imara ama mwenye nguvu bali ina maana ya kuwa na uwazi,kuhusisha watu wengine,imani na amani na pia mwelekeo wa siku za usoni Utaweza kujifunza ya kuwa huwezi kutarajia viongozi wa jamii kuwa (ama wawe) na uwazi wanapo tumia mali ya jamii ikiwa wewe mwenyewe hauna uwazi unapoendelea na shughuli au kazi yako katika jamii. Tazama kwenye: Kamusi ya maneno makuu, ili uweze kupata mwanzo wa discussion kuhusu lengo haya (kupunguza umaskini, kuendeleza jamii). Linganisha na maandishi yaloyomo kwenye shajara lako ––»«––© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
––»«–– |
Ukurasa wa nyumbani |
Matayarisho |