Tafsiri:
Akan |
Maneno muhimu that begin with the letter HMwandishi Phil BartleMtafsire: Alpha Mukama, Abdulrazzaq Adam OtienoHasira Hasira ni hisia hatari sana katika kazi yako –– tunaisindaje. Kama binadamu tuna hisia, na hasira ni moja ya hsia hizo. Ni sahihi kuwa na hasira; Tusijisikie vibaya au aibu kuwa na hasira. Hasira yenyewe ni hisia ya kawaida kwa binadamu. tunatakiwa tuikubali pale inapotutokea. Tunafanyeje tunapopata hasira? hii itatuathiri tunapoiwezesha jamii, kuratibu wanaojitolea au kuwaongoza wafanyakazi. Endapo mteja, mtu anaejitolea, mfanyakazi au mwanajamii anapofanya kosa, hasa lile ambalo litaathirishabaha zetu, kwa mfano, tunashawishika kuwa na hasira wakati huo ni muda muafaka tunaotakiwa kuwa kimya. Tunapoona mtu amefanya makosa yanayoweza kuharibu matokeo ya kazi yetu, tunapata hasira na ni jukumu letu kujitahidi kuimudu hiyo hasira. Njia mojawapo ya haraka ni kwenda matembezi. Kama hakuna muda wa kutosha, basi nenda katika chumba kingine bila kuonyesha hasira yako, na utulize hasira zako huko mbali na yule aliyekukosea. Na baada ya kutuliza hasira zako utakuwa tayari kuendelea tena na kazi iliyokuletea hasira.Kama ilisababishwa na mteja, mfanyakazi au mtu wa kujitolea chukua hatua zinazoonyeshwa kwenye maneno muhimu. Kosa Hicho kitendo kitakuwa na manufaa tu kama tutakifanya wakati tumetulia, na kujiweka sawa tena. العربيّة:غضب, বাংলা : রাগ, Bahasa Indonesia: kemarahan, Català: ira, Deutsch: wut, Ελληνικά: Θυμός, English: anger, ire, choler, Español: Ira, Euskera: Haserrea, Filipino: galit, Français: colère, Galego: anoxo, हिन्दी : क्रोध, Italiano: collera, 日本語: 怒り, Kiswahili: hasira, Malay: Kemarahan, Português: ira, Română: furie, Pyccкий: злость, Tiên Việt: sự tức giận, తెలుగు: ఆవేశము, Türkçe: öfke, 中文 : 怒气──»«──Kama umeona neno linalohusiana na uwezeshaji jamii na unataka kujadili, tafadhali tuandikie.kama utanakili maandishi kutoka kwenye mtandao huu, tafadhali mnukuu mwandishi au waandishi |
Ukurasa wa nyumbani |